in , , ,

Mkutano Arsenal pasua kichwa

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema tarehe ya Mkutano Mkuu wa
Mwaka (AGM) wa klabu hiyo si nzuri kwake, kwani utafanyika ni siku
moja tu kabla ya timu yake kushuka dimbani.

Arsenal wanakabiliana na Reading kwenye mechi ya Kombe la Ligi (EFL)
Jumanne usiku, ikimaanisha kwamba kipindi cha mwisho cha mazoezi
alichotarajia kuendesha Wenger kitaathiriwa na mkutano huo wa wana
hisa uliopangwa kufanyika saa 5.30 asubuhi Jumatatu.

Ilivyo ni kwamba Wenger mkutanoni humo anatakiwa kwa sababu amepangwa
kutoa hotuba ambayo kwa kawaida hutoa mwelekeo wa timu kwa siku zijazo
na kujadili zilizopita. Awali alionesha kana kwamba hangeweza
kuhudhuria mkutano huo.

“Kikawaida nisingetakiwa kuwa huko (mkutanoni) kwa sababu tuna mechi
Jumanne na tunafanya mazoezi Jumatatu asubuhi … sijui kama nitaenda
(mkutanoni). Kazi yangu ni kufundisha timu … nitaona nitakavyoweza
kufanya vyote viwili,” akiongeza kwamba ni ngumu kuukacha mkutano huo.

Imeelezwa kwamba mkutano huo unafanyika Jumatatu ikiwa ni mara ya
kwanza, na sababu ni kuendana na ratiba ya mmiliki wa hisa nyingi
klabuni hapo, Stan Kroenke, ambaye Jumapili hii alikuwa kwao Marekani
na alitazama mubashara mechi baina ya timu yake nyingine, Los Angeles
Rams na New York Giants huko Twickenham, Oregon.

Imekuwa kawaida wajumbe kuvutana lakini safari hii inadhaniwa
kutakuwapo utulivu, kwani timu inakwenda vyema, wakiwa nafasi ya pili,
wakifungana pointi na Manchester City. Wenger alifanikiwa pia kufanya
usajili ambao kwa kiasi fulani uliwaridhisha washabiki na wachezaji
wapya wanafanya vyema – Granit Xhaka na Shkrodan Mustafi. Wawili
wengine ni Rob Holding na Lucas Perez.

Hata hivyo, Wenger anasema kwamba hawajapata kufanya mkutano timu
ikiwa katika hali mbaya, kwani imekuwa kawaida wao kuwa katika nafasi
nne za juu. Alimwambia mmoja wa waandishi ajaribu kufanya kazi klabuni
hapo walau kwa miezi sita tu angeona jinsi hali ilivyo ndani; siku
zote tumekuwa katika hali njema kifedha.

“Labda wana hisa hawakufurahia jambo fulani. Je, itakuwa nzuri zaidi
safari hii? Njoo kwenye AGM ujionee. Mie sijui kutabiri hali ya hewa,”
akasema alipoulizwa iwapo hali itakuwaje kwenye mkutano huo.

Arsenal walipoteza nafasi ya kuwa kwenye usukani wa ligi wakati wa
mkutano huo, baada ya kwenda sare tasa na Middlesbrough Jumamosi
iliyopita na kumaliza mtiririko wa ushindi katika mechi saba mfululizo
kwenye mashindano yote.

Wenger anasema Mfaransa mwenzake, Olivier Giroud aliyekuwa majeruhi
kitambo sasa huenda akacheza mechi hiyo. Alikuwa amejeruhiwa kidole
cha mguu. Kimwili ni timamu lakini alikuwa bado hajawa sawa kabisa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Man U wamekaa vibaya

Tanzania Sports

Carlos Alberto, Brazil World Cup-winning captain, dies aged 72