in

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF ( This is an Advertisement)

Mfuko wa Pensheni wa PSPF


TANGAZO LA KUUZA NYUMBA ZA MFUKO

Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).

Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo. Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne.

Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa ilipo. Malipo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:

1) UNUNUZI KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):
Mnunuzi atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments) kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya miaka mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua nyumba (kama mpangaji).

Mpango huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini tu) na

sh. 813,000.00 (laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.

Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Mfuko wa Pensheni wa PSPF

2) MALIPO YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)
Mnunuzi atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).

3) MKOPO WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):
Mnunuzi anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB, Azania, Exim na NMB

MUHIMU! Iwapo utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.

Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au E-mail: [email protected]

Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu zilizopo katika kila mkoa.

Imetolewa na

Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Pensheni wa PSPF

20140130-144028.jpg

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man City wawanyuka Spurs 5-1

Mourinho kakosea, sio soka ya karne ya 19