in

Samatta,Watkins, majibu mwisho wa msimu..

Watkins

Wikiendi iliyopita tumeshuhudia washambuliaji wawili waking’ara kwa  kupachika mabao ya ushindi kwa timu zao. Mbwana Samatta  alikiongoza kikosi cha Fenerbahce kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Karagumruk.  

Samata alipachika mabao hayo ikiwa ni mchezo wake wa kwanza katika  Ligi Kuu Uturuki. Kocha wa klabu hiyo, Erol Bulut anaonekana kuwa  na matumaini makubwa kwa Mtanzania huyo ambaye amejiunga timu  hiyo akitokea Aston Villa.  

Baada ya kumalizika dakika 90 za mchezo, Samatta aliviambia vyombo  vya habari kuwa, ““Nina furaha kusaidia ushindi wa timu yangu kwa  kufunga mabao mawili. Ninatamani mabao hayo yawe chachu ya  kutwaa ubingwa kuliko kufunga mengine 100 bila kuchukua ubingwa  msimu huu. Nitakuwa furaha kufunga mabao, lakini kwangu timu  kufanya vizuri ni kitu muhimu zaidi,” alisema Samatta mara baada ya  mchezo wao kumalizika. 

Naye kocha Erol Bulut ameonekana kufurahishwa na umahiri wa  Samatta hasa kutokana na kupachika mabao mawili ya ushindi katika  mchezo wake wa kwanza. Hali hiyo inatajwa kuwa itamwongezea  kujiamini na sasa huenda akapachika mabao mengi.  

Tanzania Sports
Mbwana Samatta

Kwa upande mwingine, mshambuliaji Ollie Watkins alikiongoza kikosi  cha Aston Villa kuibuka na ushindi wa mabao 7-2 dhidi ya mabingwa  watetezi Liverpool. Kwenyre mchezo huo uliofanyika Villa Park, Ollie  alipachika mabao matatu na kutengeneza bao moja, Jack Grealish  alitengeneza mabao matatu na kupachika mawili. McGinn alipacgika  bao moja na kutengeneza moja. Hii ilikuwa taswira nzuri ya Ollie  kwenye kikosi cha Aston Villa.

Wikiendi hiyo vigogo wa soka Liverpool na Manchester United  vilichapwa kwa jumla ya mabao 13. Liverpool walizabwa mabao 7-2 na  Aston Villa. Man United walikung’utwa mabao 6-1 na kikosi cha Jose  Mourinho, Tottenham Hotspurs. 

Jicho langu limewatazama washambuliaji wawili, Mtanzania Mbwana Samatta na Ollie Watkins. Samata ameanza Ligi Kuu Uturuki kwa  kupachika mabao mawili wikiendi iliyopita. Wakati Ollie Watkins  alipachika mabao matatu dhidi ya Liverpool. Kwenye mchezo wa huo  Samatta amezidiwa goli moja kwenye mchezo mmoja tu. 

Baada ya mechi nne za awali za EPL zipo rekodi za timu mbili tu hadi  sasa ambazo hazijafungwa; Ni Aston Villa na Everton. Ushindi wa  Aston Villa umerudisha kumbukumbu yay a Desemba mwaka 1976  ambapo kikosi cha Liverpool kilifungwa mabao 5-1 na wababe hao wa  Villa Park. Baada ya kipigo hicho Liverpool ilifanikiwa kumaliza msimu  ikiwa bingwa wa EPL na Ulaya. 

BIASHARA YENYE FAIDA? 

Watkins
Watkins

Mshambuliaji Ollie Watkins alijiunga na Aston Villa msimu huu kuchukua nafasi ya Mbwana Samatta aliyeuzwa kwenda kwa vigogo wa  Uturuki, Fenerbahce ambao hadi anajiunga walikuwa wnashikilia nafasi  ya nane katika msimamo wa Ligi hiyo.  

Kufanya vizuri kwa Samatta na Ollie Watkins ni ushahidi kuwa  biashara iliyofanyika ni yenye faida tu, aliyeuzwa anafanya vizuri,  aliyenunuliwa kuchukua nafasi yake naye anafanya vizuri.  Aliyenunuliwa anafanya vizuri. Aliyenunuliwa Aston Villa ameongeza  morali kwenye timu sawa na Samatta aliyeongeza mabao Fenerbahce.  Vigogo hao wa Uturuki wamesajili wachezaji takribani 8 ili kuimarisha  kikosi chao akiwemo Samatta.

Dalili zinaonesha kuwa Aston Villa hawataki kurudia makosa. Kwamba  huenda likawa jambo gumu sana kushuhudia Aston Villa inashuka  daraja msimu huu.  

Mechi nne walizocheza tangu kuanza msimu huu zimeonesha namna  timu hiyo ilivyo na uchu wa kushinda kila dakika. Hasa timu hiyo  inaonekana kuwa na ari zaidi na kama vile inataka kumalizana na  mambo ya kunusurika kushuka daraja mapema. Kuwafunga mabingwa  watetezi kunaibua ari na tiba kisaikolojia kwani inawapa wachezaji  kujiamini. 

Hata hivyo uzoefu unaonesha kuwa mechi za mwanzoni na mwishoni  mwa msimu zinakuwa ngumu zaidi. hivyo katika mechi za awali  ambapo nne zimechezwa, inawezakana ikawa ari ya mwanzo wa msimu  lakini ikaleta taswira nyingine mwishoni.  

Changamoto waliyonayo Aston Villa ni kulinda kiwango walichonacho  sasa na mwishoni itathibitika nani ataibuka kuwa kinara kati ya  Watkins na Samatta. Nje ya hapo inaonekana ni biashara nzuri  kufanyika.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
AV

Je, Liverpool wanaweza kutetea taji la EPL?

wachambuzi wa soka

Korona Inavyoendelea kuwaadhibu Wachambuzi