in , , , ,

Arsenal, Man City chali Ulaya

Arsenal na Manchester City wamepoteza mechi muhimu za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), ambapo Washika Bunduki wa London wapo hatarini kutolewa.
Matumaini ya Arsenal kusonga mbele yametiwa majaribuni baada ya kubamizwa 3-1 na Monaco wa Ufaransa, tena wakiwa nyumbani. Hawajapata kufika robo fainali tangu 2010.

Arsenal walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na kiwango chao kizuri wakilinganishwa na Monaco, lakini waliduwazwa dimbani, licha ya kutawala mchezo kuliko wapinzani wao.
Monaco walikuwa wazuri katika kulinda lango na pia walishambulia vyema wakiichambua ngome ya Arsenal, wakapata bao la kuongoza kupitia kwa Geoffrey kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspur, Dimitar Berbatov kufunga la pili.

bonge la goli

Akitokea benchi, Alex Oxlade-Chamberlain alifunga bao la kufutia machozi na kabla vumbi halijatulia, Yannick Ferreira Carrasco akafunga la tatu na kuwaacha vijana wa Arsene Wenger wakishangaa.
Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim alishangilia mithili ya Jose Mourinho wa Chelsea kwa kuteleza kwa magoto uwanjani. Itabidi Arsenal wafunge walau mabao matatu kwenye mechi ya marudiano ugenini ili waweke hai matumaini ya kusonga mbele.

MAN CITY WAKWAMA KWA BARCELONA

man city

Luis Suarez amerudi England kwa mafanikio, akiwasaidia Barcelona kuwafunga Manchester City 2-1, ambapo mlinzi wa City, Gael Clichy alitolewa nje baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano kwa mchezo wa rafu.

Suarez alionesha soka safi, akiwa makini na mwenye nidhamu, baada ya uhamisho wake uliogharimu pauni milioni 75 kutoka Liverpool. City walicheza vyema kipindi cha pili na wakapata bao kupitia kwa Sergio Aguero, lakini halikutosha kuwapa ushindi, hivyo watakuwa na kazi ya ziada watakapokwenda Camp Nou kwa mechi ya marudiano.

City hawakuwa na kiungo wao wa kimataifa wa Ivory Coast, YayaToure kwa sababu ya kutumikia adhabu, na sasa ni juu ya Kocha Manuel Pellegrini kuwapanga upya vijana wake kwa ajili ya mechi ijayo ugenini.
Katika mechi nyingine Bayer Leverkusen wa Ujerumani waliwafunga Atletico Madrid wa Hispania 1-0 huku Juventus wa Italia wakiwazidi nguvu Borussia Dortmund wa Ujerumani kwa 2-1.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

MDORORO WA MPIRA WA WAVU NCHINI TANZANIA

TAIFA STARS KUSHIRIKI COSAFA CUP