in , ,

EURO 2016: NCHI KADHAA ZIMEFANYA MAAJABU KUFUZU

 

Michezo ya makundi ya kuwania kufuzu Uefa Euro 2016 inafikia tamati hapo kesho. Michezo 18 ya leo Jumatatu na kesho Jumanne itahitimisha michezo ya hatua hizo za makundi. Michuano ya Euro 2016 kwa mara ya kwanza mwakani itashirikisha timu 24 ambapo awali ilihusisha timu 16.

Uholanzi iliyowahi kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia mara tatu ipo kwenye wakati mgumu kuweza kufuzu. Timu hiyo iliyo na alama 13 kwenye Kundi A inahitaji matokeo ya ushindi pekee kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Jamhuri ya Czech huku ikiomba dua Uturuki wenye alama 15 wapoteze dhidi ya Iceland ndipo iweze kujiweka kwenye nafasi ya kufuzu.

Timu hiyo iliyo na alama 13 kwenye Kundi A inahitaji matokeo ya ushindi pekee kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Jamhuri ya Czech huku ikiomba dua Uturuki wenye alama 15 wapoteze dhidi ya Iceland ndipo iweze kujiweka kwenye nafasi ya kufuzu.

Uturuki waliokuwa washindi wa tatu kwenye Kombe la Dunia 2002 na kutinga nusu fainali Euro 2008 wanahitaji angalau sare kwenye mchezo wa leo dhidi ya Iceland lakini hawatakuwa wamefuzu moja kwa moja kwenye hatua za makundi za Euro 2016 hata kama watapata ushindi.

Sare wanayoihitaji ni kwa ajili ya kuwawezesha kubakia kwenye nafasi ya tatu kwenye Kundi A ili waingie kwenye hatua inayofuata ya michezo ya mtoano kwa ajili ya kukata tiketi ya kuingia kwenye hatua za makundi za Euro 2016.

Ugiriki waliotwaa taji la Euro 2004 baada ya  kuwafunga Ureno bao moja kwa sifuri kwenye mchezo wa fainali wanaburuza mkia kwenye Kundi F na nafasi yao ya kufuzu ilishapotea tangu Septemba 4 walipofungwa nyumbani 1-0 dhidi ya Finland.

Advertisement
Advertisement

Serbia walio kwenye Kundi I pia walishashindwa kufuzu. Wamekusanya alama nne pekee kwenye michezo yao yote nane kwenye kundi hilo. Serbia wamewahi kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mara 11 ikiwemo ile ya 2010 na pia wameshiriki michuano ya Euro mara 5 huku wakitinga fainali mara mbili.

Wakati Ugiriki na Serbia wakishindwa kufuzu na mataifa kama Uholanzi na Uturuki ambayo yana historia ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa soka yakihangaika kutafuta nafasi ya kufuzu Uefa Euro 2016 kwenye michezo ya mwisho inayopigwa leo na kesho, tayari kuna timu kadhaa zimeshafuzu mapema kwa namna ya kustaajabisha ama kinyume na matarajio ya wengi.

Iceland ni taifa changa na lisilo na historia yoyote ya kutukuka kwenye mchezo wa soka. Hata hivyo kwa sasa ni vinara wa Kundi A na walishafuzu tangu Septemba 6 walipotoa sare ya bila kufungana dhidi ya Kazakhstan. Timu hii imefanya maajabu kwa kuwa hii ni mara ya kwanza inakata tiketi ya kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa. Kwenye safari yao ya michezo ya kufuzu wamefanikiwa kuwafunga Uholanzi nyumbani na ugenini.

Eden Hazard, akifurahia ushindi, baada ya kufunga penati moja na kukosa nyingine..
Eden Hazard, akifurahia ushindi, baada ya kufunga penati moja na kukosa nyingine..

Wengine waliofuzu mapema na kuwastaajabisha watu ni Wales ambao bado wamebakiza mchezo mmoja. Mara ya mwisho Wales walipopata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa ilikuwa mwaka 1958 waliposhiriki Kombe la Dunia. Kwa sasa wakiwa na alama 18 wanashika nafasi ya pili kwenye Kundi B nyuma ya Ubelgiji wenye alama 20. Pengine mafanikio ya Wales yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mchezaji ghali zaidi duniani Gareth Bale.

Albania pia wamefanya maajabu. Ushindi wa mabao matatu kwa sifuri walioupata hapo jana dhidi ya Armenia umewahakikishia nafasi ya pili kwenye Kundi I wakiwa na alama 14 nyuma ya vinara Ureno walio na alama 21 na hivyo wamefuzu moja kwa moja kwenye hatua za makundi za Uefa Euro 2016. Nao pia hii ni mara ya kwanza wanafanikiwa kupata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa.

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Taifa Stars wavuka

Tanzania Sports

JURGEN KLOPP HAWEZI TENDA MIUJIZA