in , , ,

Dirisha la usajili kiangazi lasogezwa mbele

Hatimaye imekubaliwa kwamba kuanzia kiangazi mwaka huu, Dirisha la Usajili wa Ligi Kuu ya England (EPL) litafungwa Septemba mosi kama ilivyo kwa nchi nyingine za Ulaya.

Hii itamaanisha kwamba dirisha hilo litafungwa wakati msimu wa ligi kwa 2020/2021 ukiwa umeshaanza, hivyo kutoa muda zaidi kwa klabu za England kuendelea na usajili tofauti na awali ambapo lilifungwa mapema.

Klabu za England zilikuwa zikipata tabu kwa kushindwa kusajili wachezaji baada ya msimu kuanza, lakini zikawa na bahati mbaya pia kwamba wachezaji wao bado wangeweza kuchukuliwa na klabu za nje ya England.

Hiyo itabaki historia, kwa sababu sasa watakwenda sambamba na klabu za ligi nyingine kubwa barani Ulaya, dirisha likifungwa saa tano usiku wa Septemba mosi. Klabu zilipiga kura kwa wingi kukubaliana na dirisha jipya litakavyokuwa kuanzia mwaka huu.

Klabu zilihisi kwamba ufungwaji mapema wa dirisha la usajili msimu wa kiangazi ulivuruga mipango na ufanisi wao mwanzoni mwa msimu. Klabu nyingi, hasa zile sita kubwa zilishalalamikia hali hiyo kwa muda sasa.

Kipekee, Manchester United na Tottenham Hotspur zililalamikia kushindwa kuweka sawa mambo yao ya usajili kiangazi kilichopita. Spurs, kwa mfano, walitaka kumuuza Christian Eriksen, lakini wakashindwa kwa sababu walikosa mbadala wake ndani ya muda wa dirisha la usajili la England.

Eriksen alilazimika kubaki na Spurs hadi Januari mwaka huu alipohamia Internazionale, Italia. Uamuzi wa kubadili muda wa dirisha hilo, kwa maana ya kupeleka mbele kuanzia kiangazi cha mwaka huu ulikubaliwa kwenye mkutano wa kawaida wa wadau, ukipitishwa kwa wingi wa kura za kawaida.

Msimu wa EPL mwaka huu utaanza Agosti 8, zikiwa ni wiki nne baada ya michuano ya fainali za Euro 2020. Mwenyekiti wa Liverpool, Tom Werner, anasema kwamba walihisi ni vyema kwa klabu nyingi kuidhinisha mpango huo na kwenda sambamba na ligi nyingine, badala ya kujinyima fursa ya kuweka mambo ya usajili sawa.

“Ilikuwa (tarehe ya mapema ya kufunga dirisha la usajili) inatupa shinikizo kubwa kwetu sote katika kufikia uamuzi na ikawa inawapa faida klabu kwenye ligi za nchi nyingine, kwa ihiyo ni vyema sote kuwa pamoja,” anasema Werner.

Mwenyekiti huyo akasema pia haoni kwamba kuna haja ya kulazimisha klabu kuwa na sehemu kubwa ya wachezaji wa ndani, kwani ni sehemu ambayo wachezaji wazuri hupenda kuingia na kufanya hivyo kutafisha ubora wa ligi yenyewe.

Chama cha Soka (FA) kimekuwa kikitaka klabu kusajili zaidi wachezaji raia wa Uingereza au waliokulia humu. Mjadala mpya unaanza baada ya Uingereza kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya (EU), jambo linaloonekana litasababisha mabadiliko ya sheria na kanuni muda si mrefu ujao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

EPL na mjadala wa wachezaji wa kigeni

Tanzania Sports

Arsenal wanaweza kurudi Ligi ya Mabingwa Ulaya