in , , ,

Blatter alazwa hospitali

 

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Sepp Blatter amelazwa hospitalini kutokana na kupatwa mshituko wa neva.

Blatter (79) aliyesimamishwa kwa siku 90 kujishughulisha na masuala ya soka wakati akichunguzwa kwa kashfa ya kutoa mlungula, alilazwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya lakini sasa imeelezwa atakaa zaidi humo.

Mwanamichezo huyo aliyeongoza ulimwengu wa soka kwa miaka 18 sasa, awali ilidaiwa alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo hivyo ikabidi apate huduma ya matabibu, sasa imebainika ana tatizo la mshituko wa neva.

Awali, mwanasheria wake, Richard Cullen alieleza juu ya uangalizi huo wa madaktari kutarajiwa, lakini akawa amesema alitarajia arejee nyumbani mapema kabla hali kubadilika na kutolewa maelezo tofauti.

Hata hivyo, maswahiba wake wameeleza kwamba hali yake si mbaya na anatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida japokuwa atabaki hospitalini hadi mapema wiki ijayo. Blatter amesimamishwa kazi hizo sambamba na Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa), Michel Platini kwa tuhuma za makosa yanayohusiana.

Advertisement
Advertisement

Imeelezwa kwamba Blatter amekuwa katika kupambana dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Fifa kumsimamisha kazi na alinukuliwa akiwaambia rafiki zake kwamba hakuna kamati yoyote ile inayoweza kumweka nje ya utawala wa Fifa.

Msaidizi wake, Walter Gagg, amesema kwamba bosi huyo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa hafla ya kukabidhi tuzo ya Mwanasoka Bora – Ballon d’Or jijini Zurich, Januari 11 akimaanisha kwamba atakuwa timamu lakini pia hana doa kuhusu tuhuma anazohusishwa nazo.

Katikati ya sakata hilo ni shauri la jinai linalomlenga Blatter na Platini, kwamba Blatter alitumia vibaya pauni milioni 1.35 kumpa Platini kama hongo mwaka 2011 ili ajitoe kwenye kugombea urais wa Fifa wakati huo.

Wawili hao wanakana, wakidai hayo yalikuwa malipo halali kwa Platini, kutokana na kazi ya ushauri wa ufundi kwa rais huto wa Fifa aliyokuwa ameifanya. Inashangaza kuona kwamba malipo yalifanyika karibu mwaka mzima baada ya kazi kumalizika, na muda mfupi tu kabla ya uchaguzi wenyewe ambao Platini alijiondoa mara na Blatter akashinda.

Uchaguzi wa rais unafanyika Februari mwakani, baada ya Blatter aliyechaguliwa tena Mei mwaka huu kuamua kuachia ngazi wakati huo ukifika, kwa maelezo kwamba si ulimwengu wote wa soka unaomuunga mkono.

Hata hivyo, kwa wakati huu Blatter amekuwa ofisini akiendeleza kile anachoita mchakato wa mageuzi makubwa ndani ya shirikisho hilo. Platini amejitosa safari hii kuuwania urais ila haijajulikana iwapo marufuku ya kushiriki michezo itaondolewa kabla ya mchakato wenyewe kuanza.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Kashfa riadha yashika kasi..

Tanzania Sports

STARS v. ALGERIA: TUJITUME DAKIKA TISINI