in , , , ,

Advocaat bosi mpya Sunderland

Klabu ya Sunderland wamemteua Dick Advocaat kuwa kocha wao mpya, akipewa jukumu la kuwaokoa dhidi ya kushuka daraja.
Kocha huyu wa zamani wa Uholanzi amepewa kazi hiyo hadi mwisho wa msimu, na ameahidiwa pauni milioni moja akifanikisha kuwabakisha juu.

Sunderland walio pointi moja tu kutoka eneo la kushuka daraja walitangaza kumfukuza kazi kocha wao, Gus Poyet aliyewaokoa kushuka daraja msimu uliopita.
Mwenyekiti wa Sunderland, Ellis Short amesema kwamba lengo lao kwa sasa ni moja tu, kuhakikisha timu inazoa pointi na kuondoka eneo la kushuka daraja.

Advocaat mwenyewe amesema ana hamu ya kuanza kazi hiyo katika klabu aliyosema ni kubwa. Akiwa na umri wa miaka 67, Mholanzi huyu ana uzoefu na huenda akafanikisha kazi, na hivyo atapata bonasi ya pauni 500,000 akishamaliza.

Inaelezwa kwamba uongozi wa Sunderland ulikuwa ukitafakari kupata kocha mzoefu na mwenye mbinu za kuwavusha kutoka walipo, ambapo alifikiriwa pia kocha wa zamani wa Manchester United,Sir Alex Ferguson.

Lengo ni hadi mwishi wa msimu tu, ambapo watatafakari kocha mwingine wa kuendeleza gurudumu hilo. Poyet amefukuzwa baada ya kufungwa 4-0 nyumbani kwao na Aston Villa ambao pia wanapambana kuepuka kushuka daraja.

Advocaat ataanza mtihani wake kwa mechi dhidi ya West Ham Jumamosi hii. West Ham nao wanadaiwa kufikiria kumbadili kocha Sam Allardyce iwapo hatakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi mbili hivi zijazo.

Advocaat aliwaongoza Zenit kutwaa ubingwa wa Uefa 2008 walipocheza fainali dhidi ya Rangers jijini Manchester. Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza kufundisha timu ya ligi kuu ya England.
Amepata kuwafundisha Rangers wa Uskochi kati ya mwaka 1998 na 2002. Alitwaa ubingwa wa Uholanzi na Kombe la Ligi mara mbili akiwa Ibrox, lakini pia ubingwa akiwa na PSV Eindhoven nyumbani kwao kama ilivyokuwa kwa Zenit St Petersburg nchini Urusi.

Amefundisha Timu ya Taifa ya Uholanzi katika vipindi viwili tofauti na pia amefanya kazi Emarati, Korea Kusini, Ubelgiji na Serbia. Aliachia ngazi Serbia baada a kufungwa 3-1 na Denmark katika mechi za kufuzu kwa Euro 2016.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Kutoka TFF leo……

Klabu za England kwa heri Ulaya