in , , ,

Sunderland wamfukuza kocha O’Neill

Klabu ya Sunderland inayoteremka hatua kwa hatua kuelekea kushuka daraja, imemtimua kocha wake, Martin O’Neill.
Hatua hiyo ambayo haikutarajiwa, imekuja muda mfupi tu baada ya timu hiyo kupambana kiume na kupoteza mechi dhidi ya Manchester United kwa 0-1.
Klabu hiyo inayojulikana pia kwa jina la ‘Black Cats’ imesema kwamba hatua hiyo imechukuliwa kutokana na mwenendo wa timu, ambapo sasa inashika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi.
Sunderland wenye pointi 31 wamemshukuru O’Neill kwa kazi aliyofanya tangu ajiunge nao 2011 na kuongeza kwamba mrithi wake atatangazwa katika siku zijazo.
Huyu ni kocha wa tano kufukuzwa kazi na klabu ya Ligi Kuu ya England, baada ya Roberto Di Matteo wa Chelsea na Mark Hughes wa Queen Park Rangers (QPR).
Wengine walioonja joto ya jiwe ya waajiri wao ni Brian McDermott wa Reading na Nigel Adkins wa Southampton aliyechukuliwa na Reading wiki iliyopita.
Sunderland iliyokuwa na kawaida ya kuanza ligi na kumalizia kwenye nafasi za katikati, imepoteza mwelekeo msimu huu, ambapo majuzi, ambao imebakisha pointi moja kuingia eneo la kushuka daraja.
Wigan na Aston Villa zilizo nyuma yake, zina pointi 30 lakini zina mchezo mmoja mkononi, hivyo kuna uwezekano wa mzunguko ujao Black Cats wakaingia rasmi eneo la hatari.
QPR na Reading wana pointi 23 kila moja, Reading wakishika mkia kwa uwiano mbovu wa mabao, lakini pia QPR wakiwa na mechi moja mkononi.
Pamoja na kumwondoa O’Neill, bila kujali kocha gani atachukua usukani Stadium of Light, kaskazini mashariki mwa England, kwani wamebakisha mechi ngumu.
Katika mechi ijayo, Sunderland watakwaana na Chelsea Stamford Bridge, kisha kwenda kwa jirani zao Newcastle kabla ya kuwakaribisha Everton.
baada ya hapo watawakaribisha wagumu wengine, Stoke City, kisha watabaki hapo hapo kucheza na Southampton wenye ufufuko mpya kabla ya kumalizana na Tottenham Hotspurs.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Panga la UEFA kwa England?

Liverpool wawavurugia Aston Villa