in , , , ,

Suarez safi Barca lakini …

*Wakili wake akimbilia Cas

Barcelona wamekamilisha usajili wa Luis Suarez kutoka Liverpool baada ya kulipa ada ya pauni milioni 75.
Hata hivyo, utata uliopo sasa ni iwapo wataruhusiwa kumtambulisha Suarez Camp Nou kwa washabiki wao kama walivyofanya kwa wachezaji wengine, kama Neymar, Cesc Fabregas ,  Zlatan Ibrahimovic na David Villa.

Hiyo inatokana na uamuzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kumfungia mshambuliaji huyo wa Uruguay kujihusisha na shughuli zote za soka kwa miezi minne baada ya kumng’ata mchezaji wa Timu ya Taifa ya Italia, Giorgio Chiellini.

Baadhi ya wajuzi wa sheria wanasema kutambulishwa kwake uwanjani ambapo maelfu ya washabiki huhudhuria au kufanya mkutano na wanahabari kutakuwa kinyume na kufungiwa kwake na kunaweza kuongeza adhabu.

Hata hivyo, mwanasheria wake, Alejandro Balbi amesema kwamba wanakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) na matarajio yake ni kwamba adhabu hiyo aliyodai ni ya kizamani, kikatili na kifashisti itafutwa.

Wanaweza pia kuwauliza Fifa iwapo wanaweza kumtambulisha mchezaji wao huyo mpya na aghali atakayeungana na akina Neymar, Messi na wengineo Oktoba mwaka huu kwenye La Liga.

Suarez (27) alikosa mechi kadhaa za mwisho za Ligi Kuu England msimu wa 2012/13 na za mwanzo za 2013/14 kwani alikuwa akitumikia adhabu ya Chama cha Soka cha England kwa kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic wakati akiwa Liverpool.

Mbali ya kupigwa marufuku kucheza miezi mine, Suarez pia amezuiwa kucheza mechi tisa za kimataifa, kulipa faini ya dola 66,000 na rufaa hiyo ikikatwa kweli inaweza kuwa jaribio kubwa la kutikisa au kupunguza nguvu za Fifa iliyokataa rufaa ya mchezaji huyo wiki hii.

Suarez alikana kumng’ata Chiellini akisema waligongana meno yakamuumiza lakini kwamba hata yeye aliumia. Baadaye alimwomba radhi Mtaliano huyo. Baada ya kumng’ata Ivanovic aliomba pia radhi na kuahidi kutorudia tena tabia hiyo mbovu.
 
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Brazil wajaribu kufuta machozi

Fifa yataja wanaowania tuzo