Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhamini na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo imeanza mazoezi katika uwanja wa Addis Ababa zamani ukifahamka kama (Haille Sellsie) uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 14, jijini Alexandria.

Stars ambayo iliwasili jana jioni jijini Addis Ababa imefikia katika hoteli ya Debre Damo iliyopo eneo na 22 Mazoiria ambapo itakaa kambi kwa kipindi cha wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema anashukuru vijana wake wamefika salama, na wapo katika hali nzuri, anaamini wiki moja ya maandalizi nchini Ethiopia itasaidia kikosi chake kuwa fiti ajili ya mchezo.

Akiongelea kuhusu kambi, kocha Nooij amesema kwa kuwa mji wa Addis Ababa upo katika ukanda wa juu( mita 2000 kutoka usawa wa bahari), kambi ya mazoezi itakua nzuri kutokana na wachezaji kufanya mazoezi katika hali hiyo na kwenda kucheza katika ukanda wa kawaida.

Kuhusu hali ya hewa ni nzuri kwani baridi iliyopo kwa sasa Addis Ababa ni ya kawaida, hivyo haitaweza kuwasumbua wachezaji katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.

Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa katika jiji la Alexandria ambalo lipo eneo la bahari ya Mediteranian.

NB: Picha za mazoezi ya Taifa Stars leo zimeambatanishwa.

Napatikana kwa namba hii Ethiopia +251 96100 5754

TFF YAWAITA SIMBA, SINGANO JUNI 9

Singano
Singano

TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano na klabu ya Simba.

TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Ramadhani Singano wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.

Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.

Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

PSPF YADHAMINI UZINDUZI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII YA WANAFUNZI WA IFM

MGOGORO WA MLUNGULA FIFA