Young Africans

Young Africans

Kikosi cha timu ya Yanga
Kikosi cha timu ya Yanga

Yanga ndiyo klabu kongwe kuliko zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2014/15.
Ilianzishwa mwaka 1935 jijini Dar es salaam.
Ni moja ya timu kubwa, kongwe na maarufu Tanzania na pia ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara mara 24.
Ndiyo inayoongoza kwa kuchukua ubingwa mara nyingi kuliko timu nyingine yoyote Tanzania Bara.
Mafanikio wa klabu hiyo kwenye mechi za kimataifa ni kucheza robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika mara mbili, 1969 na 1970.
Katika hatua zote hizo mbili, Yanga ilitolewa na Asante Kotoko ya Ghana.
Moja kati ya mechi hizo 1969, ilitolewa kwa njia ya kurusha shilingi baada ya matokeo ya jumla ya mechi ya nyumbani na ugenini kuwa bao 1-1.
Wakati huo sheria ya mikwaju ya penati ilikuwa haijaanza kutumika.
Mwaka 1998, pia ilifanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi ya Klabu bingwa Afrika.
Imetwaa kombe la Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kagame Cup mara tano. Ni klabu yenye mashabiki wengi nchini Tanzania.

Vodacom Premier League. Follow Your Team