Stand United

Stand United

Stand UnitedStand United

 

Ni timu iliyoanzishwa mwaka 2012 na makonda, wapiga debe, mawakala na madereva wa stendi ya zamani na mpya ya mabasi ya kwenda mikoani na wilayani, huko mkoani Shinyanga.

 

Hawa ndiyo waanzilishi ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya timu hiyo ifike hapo ilipo.

 

Ilianza kuwa kuchangishana wenyewe, lakini baadaye ilianza kupata wafadhili pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya na mkoa ambao walijitokeza kuipa sapoti ilipokuwa inazidi kufanya vizuri.

Hivi sasa imeondokea kuwa timu kipenzi cha mashabiki wengi wa soka mkoani humo.

 

Hadi sasa inapoendelea na Ligi Kuu, ina baadhi ya wachezaji ambao ni makonda, madereva na wapiga debe na wanaendelea na kazi zao kama kawaida wanapomaliza mazoezi, mechi na kurejea kutoka mikoani kwenye mechi za Ligi Kuu.

Vodacom Premier League. Follow Your Team