Ndanda

Ndanda

Ndanda official

Ni timu mpya iliyopanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Ilianzishwa Machi 2011 huko mkoani Mtwara ambako ndiko makao makuu ya klabu hiyo, Kusini mwa Tanzania.

Timu hii ilianza kama masihara kwani baadhi ya maeneo ya shule ya msingi Ndanda waliamua kuanzisha timu ili tu kuleta ushindani na timu ziliyokuwepo hapo maeneo jirani ikijulikana kama Sokoni FC na Bodaboda FC.

Ilianza kutoa upinzani mkali kwa timu hizo pamoja na timu ya kiwanda cha Maji cha Ndanda pale ilipofanikiwa kuwaa kombe la kugombea jezi na mipira miwili mbele ya timu hizo mwaka huo huo ilipoanzishwa.

Viongozi wa klabu hiyo wakaona sasa ni wakati muafaka wa kucheza Ligi daraja la nne Wilaya ya Masasi na kuendelea vizuri.

Mwaka 2013 walifanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza, lakini hakufanikiwa kupanda Ligi Kuu, hadi msimu huu ndipo walipopata nafasi hiyo.

Vodacom Premier League. Follow Your Team