Mtibwa Sugar

Mtibwa Sugar

mTIBWA

Ni timu iliyoanzishwa mwaka 1988 na kikundi cha wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa, kilichoitwa Mtibwa Estates Ltd.

Makao makuu wa klabu hiyo yapo maeneo ya Mvomero, Turiani, mkoani Morogoro.

Ilianza kushiriki ligi daraja la nne mwaka 1989 na kupanda Ligi daraja la Kwanza mwaka 1996 ambayo mwaka 1998 ilibadilishwa na kuitwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mwaka 1998, kiwanda hicho kilinunuliwa na kampuni ya Tanzania Sugar Industry pamoja na timu ya mpira na kuanza kuchukua nyota mbalimbali kutoka timu kubwa za Simba, Yanga, kiasi cha kuifanya kuwa tishio.

Mafanikio ya juu kwa timu hiyo ni kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1999 na 2000.

Lakini pia ndiyo timu iliyotoa wachezaji wengi kwa sasa wanaocheza Ligi Kuu kwenye klabu mbalimbali nchini Tanzania.

Vodacom Premier League. Follow Your Team