Mbeya City

Mbeya City

Mbeya City Fc

Timu hii ilianzishwa kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka 2011.

Makao makuu ya klabu hiyo yako mjini Mbeya.

Timu hii inamilikiwa na Halmashauri ya jiji mkoani humo.

Inasemekana kuwa Mbeya City ni matokeo ya timu ya Rhino Football Club ya Arusha ambayo ilinunuliwa na Halmashauri hiyo na kuibatiza jina mkoa huo ikiwa daraja la kwanza Tanzania Bara.

Ilipanda Ligi Kuu msimu wa 2013/14 na kuwa timu ya kuogopwa na timu zote zilizoshiriki ligi, zikiwemo Simba na Yanga.

Ni timu iliyoleta mapinduzi makubwa kwenye soka la Tanzania kwa kukusanya mashabiki wengi wanaosafiri na timu hiyo kila wanapowenda kucheza mechi.

Mafanikio yao makubwa ni kukamata nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu 2013/14, ikiwa ni msimu wao wa kwanza tu tangu kupanda.

Vodacom Premier League. Follow Your Team