Azam

Azam

Kikosi cha Azam Fc
Kikosi cha Azam Fc

Kwa sasa ndiyo mabingwa watetezi ambayo wanafanya kila njia kuhakikisha wanalibakisha kombe mikononi mwao.
Azam FC ilianzishwa rasmi Juni 11, mwaka 2007. Hata hivyo timu hiyo ilikuwepo tangu mwaka 2004 ikiwa chini ya wafanyakazi wa kampuni ya Mzizima Flour Mill, kampuni tanzu ya Bakhresa, makao yake makuu yakiwa Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.
Timu hiyo iliitwa Mzizima FC na lengo lilikuwa ni kuwafanya wafanyakazi kujiweka vizuri kiafya.
Ilishiriki ligi daraja la tatu, Manispaa ya Ilala hadi mfumo huo wa madaraja ulipoondolewa mwishoni mwa mwaka 2005.
Baadaye Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhresa, Abubakar Bakhresa, aliona ni vyema timu hiyo ihusishe wafanyakazi wa kampuni zote za Bakhresa, na kutumia jina la moja ya bidhaa zao kubwa, Azam.
Ilipanda rasmi Ligi Kuu msimu wa mwaka 2008/09.
Msimu wake wa nne tangu itinge Ligi Kuu,  kwa misimu mwili mfululizo ilifakikiwa kumakamata nafasi ya pili, na msimu wa 2013/14 ikaingia katika historia ya kuwa miongoni mwa timu chache zilizowahi kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara.

Vodacom Premier League. Follow Your Team