D Lznzx Aaqrnm

Soka ya Afrika siku ya tano

MATAIFA ya Afrika yanaendelea na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri, ambapo mabingwa wa mara mbili, Ivory Coast walifanikiwa kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini. Tunisia waliambulia alama moja baada ya kwenda sare na Angola wakati Mali waliwashinda kwa mabao mengi walioingia kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo – Mauritania.

Mabingwa watetezi, Cameroon wanaingia uwanjani leo kwenye mechi za Kundi F kuchuana na mabingwa wa mara nne, Ghana kwenye kipute jijini Ismailia, na ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa sana.

Cameroon au Simba Wasiofugika, wanafundishwa na kiungo wa zamani wa Real Madrid na AC Milan, Clarence Seedorf – wanacheza dhidi ya Guinea-Bissau.The Black Stars, au Ghana, wakitaka kumaliza kiu ya miaka 37 bila ubingwa huo, wanakabiliana na Benin ambao ni mara ya kwanza kuingia kwenye michuano hii.

Andre Onana wa Cameroon alikuwa sehemu muhimu ya klabu ya Ajax waliotwaa mara mbili ubingwa wa Udachi na walifika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushangaza wengi kwa kuwapiga Juventus.

Onana (23) anahusishwa na kujiunga na Manchester United na leo wadau wengi watakuwa wakimwangalia jinsi anavyocheza akiwa golikipa ambaye hajaachia bao katika mechi 26 kati ya 55 alizochezea klabu hiyo hadi sasa.

Man U wanataka kupata kipa mwingine kutokana na kuzorota kwa kipa wao David de Gea kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita. Kwa upande wa Ghana, kati ya wengine, watu watakuwa wakimwangalia kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey mwenye umri wa miaka 26.

Comments