in ,

SOKA LA WANAWAKE LIMEKUWA TANZANIA

Twiga Stars

DUNIA IKISHEREHEKEA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

Machi 8 kila mwaka kiulimwengu huwa ni maadhimisho ya kimataifa ya siku ya wanawake duniani. Siku hii huadhimishwa kwa kufanywa matukio mbalimbali yenye lengo la kuonyesha nafasi ya mwanamke duniani kwa muktadha wa mwaka huo. Mwaka huu halikadhalika kumefanyika maadhimisho kwa staili yake na kila mahala kumekuwa na jumbe zake kwa mujibu wa taratibu za eneo husika walizojiwekea.

Ushiriki wa michezo kwa wanawake umekuwa kwa kiasi Fulani ingawa hakuna takwimu rasmi za ushiriki wao kwenye michezo nchini Tanzania. Ushiriki wao unaanzia kwenye uongozi mpaka uchezaji wa michezo mbalimbali. Mchezo wa Netbal (mpira wa pete) bado ndio mchezo ambao ushiriki wake umekuwa kwa kiwango kikubwa umekuwa wa wanawake. Mchezo wa mpira wa pete uongozi wake wote katika kamati tendaji bado unaongozwa na wanawake shupavu kama mwanamama Judith Ilunda ambaye amesimama katika nafasi ya katibu mkuu na michezo mingine bado ushiriki wa wanaume ndio mkubwa. Kwenye mchezo wa ngumi hakuna mwanamke ambaye amechomoza kwa kipindi hichi karibuni licha ya kwamba mwamko wa mchezo huo umekuwa mkubwa katika siku za hivi karibuni. Mchezo wa gofu kwa nchini Tanzania ushiriki wa wanawake umeongezeka na hili laonekana kwa ushiriki wao katika mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yanaandaliwa.

Katika mchezo wa riadha ushiriki wa wanawake umekuwa ni mkubwa sana kwa siku zinavyozidi kusonga. Ushiriki wa wanawake katika mbio za barabarani yaani “MARATHON” ni mkubwa sana kwani nimekuwa naona wanawake wengi sana wakijitokeza katika ya mbio hizo mbalimbali ambazo nimekuwa nashiriki. Ushiriki wao unaanzia katika uandaaji wa matukio yenyewe kwani katika kamati za uandaaji wa matukio hayo kwa kiasi kikubwa umekuwa ni uwepo wa wanawake ndio chachu ya mafanikio. Mfano mdogo ni mbio za tamasha la USHOROBA ambalo limefanyika hivi karibuni katika wilaya ya Kisarawe ambalo liliandaliwa na mkuu wa wilaya hiyo mheshimiwa Jokate Mwegelo liivyofana na kupendeza. Katika mchezo wa mpira wa kikapu ushiriki wa wanawake umekuwa ni mkubwa na hivi karibuni katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika katika mji wa Dodoma ambayo yaliyodhaminiwa na benki ya CRDB tumeona ushiriki wa wanawake katika mashindano hayo kuwa ni mkubwa kwani kulikuwepo na timu za wanawake katika mashindano hayo.

Katika muktadha wa soka nchini Tanzania limekuwa sana kwani limefikia hatua ya kuwa na ligi kuu ya wawanawake kwa upande wa Tanzania bara ambayo inashirikisha vilabu vya Yanga Princess, Alliance Girls, JKT Queens, Mlandizi Queens, Simba Queens, TSC queens, Ruvuma Queens, Kigoma sisters, Mapinduzi Queens, Tanzanite SC, ES unyanyembe pamoja na Baobab Queens.

Ligi ya soka la wanawake imeibua vipaji kadhaa ambavyo vimeonekana na kuonyesha ishara ya mafanikio katika soka hilo kwa siku za usoni. Miongoni mwa vipaji hivyo ni wafungaji mahiri ambao imezalisha ikiwemo wafungaji mahiri kama vile Asha Rashidi wa JKT queens, Oppah Clement wa Simba quens, Fatma Mustapha waJKT queens ambaye ndiye kinara wa kufunga mabao ya hat tricks katika ligi hiyo ambaye mpaka sasa ana hat trick 8 katika ligi hiyo, Aisha Juma wa Alliance Girls na Amina Ramadhan wa Ruvuma Queens.

Licha ya uchezaji hata katika uendeshwaji wa vilabu vya soka kumekuwa na ongezeko la wanawake katika nafasi za kiuongozi na kiutendaji. Vilabu kadhaa vya soka katika benchi la ufundi kuna watendaji wanawake hususani katika vipengele vya utabibu. Klabu bingwa ya soka Tanzania Simba SC imekuwa ni mfano kwa kuwa ni kilabu cha kwanza nchini Tanzania kuteua mkurugenzi mtendaji ambaye ni mwanamke baada ya kumteua mwanamama Barbara Gonzalez kuwa ndiye msimamizi mkuu wa kilabu hicho. Na kilabu hicho kimempa kibarua meneja mradi mkuu wa kilabu hicho mwanamama Belinda Paul na nafasi ya Mhasibu kuwa ni mwanamama Lucy Mng’ong’o.

Kiulimwengu katika mchezo wa soka kwa mujibu wa jarida la mtandaoni la INSIDER mchezaji wa soka ambaye analipwa pesa nyingi ni mchezaji wa timu ya USWTT aitwaye Carli Lloyd. Mchezaji huyo anakadiriwa kupokea mshara wa kiasi cha dola za kimarekani 518,000 kwa mwaka. Kipato hichi kilivyokuja kuwekwa wazi kilizusha mjadala juu ya pengo la vipato baina ya wanamichezo wa kike na wanamichezo wa kiume. Mwanamichezo huyo anazidiwa mara mara 272 ya kipato ambacho anakipata mchezaji Lionel Messi wa Barcelona ambaye kwa mwaka hukusanya kipato cha Zaidi ya dola za kimarekani milioni 141. Yaani kwa lugha nyepesi Carli Lloyd kiasi anacholipwa ni sawa na asilimia 0.3/% ya kiasi ambacho anachopokea Lionel Messi. Hali hii imepelekea baadhi ya mataifa kuanza kujadili hali hii na harakati zimeanza kupambania kutatua tatizo hili. Mataifa ya brazil na Sierra  Leone hivi karibuni yametangaza wazi kwamba wachezaji wa mpira wa mguu wanatakiwa walipwe sawa yaani malipo ya wachezaji wa soka wa kike yawe sawa na wa kiume. Tamko hili limewahi kutolewa na mataifa ya Australia, Uingereza, Norway, na New Zealand.

Hakika ni wazi ushiriki wa wanawake umekuwa nunakuwa siku hadi siku na ushiriki wao utakuwa Zaidi kama wadau Zaidi watajitokeza na kuwainua na kutoa sapoti kwa wanamama ambao wanajitoa kwa ajili ya maendeleo ya michezo ya wanawake hususani soka.

Report

Written by Kahema Fimbo

Mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uzoefu wa kuandika kuhusu habari za michezo anayeishi Dar es salaam Tanzania. Ana uzoefu wa miaka 2 wa kufanya kuandika na kasha kuchapisha Makala zake katika mitandao kadhaa nchini Tanzania. Ni mpenzi na pia ni mdau wa michezo. Amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye vyama vya michezo nchini Tanzania ikiwemo katibu mkuu taifa chama cha mchezo wa kabaddi Tanzania (Tanzania kabaddi sport association), mwenyekiti kamati ya habari chama cha shule za michezo Tanzania (Tanzania sport centres and academies association- TASCA) na pia makamu mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mkuranga( Mkuranga district football association- MDFA).
Nje ya michezo ni mwanajamii na amewahi kujitolea na pia kuwa kiongozi katika taasisi mbalimbali nchini Tanzania za vijana kam vile YOA, TYVA, YUNA, na kadhalika.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Marco Rose

Borussia Dortmund mikononi mwa Marco Rose

Rangers

Steven Gerrard yuko tayari kuwanoa Liverpool?