in

Simba Itaweza Kariakoo ‘Derby’?

Bernard Morrison

Timu ya Simba inaendelea kutimua baadhi ya viongozi wake wakiamini kuwa huenda ndio tatizo la kukosa matokeo mazuri ndani ya timu hiyo.

Timua timua hiyo naiangalia kwa jicho la pili katika kuelekea mchezo wao wa ligi ambao umepangwa kuchezwa Novemba 7 katika ratiba japo kuna hatihati ya kuubadilisha kwa mara nyingine.

Hali inavyoonekana sio shwari katika timu hiyo, huku bado anatafutwa mchawi nani, kama wakiendelea na mitafaruku hadi kufikia mchezo wao dhidi ya Yanga itakuwa balaa sana.

Japo miongoni mwa mechi ambazo huwa hazinaga mwenyewe ni huu wa watani wajadi wanapokutana kila mmoja anakuwa na jambo lake na anakamia kwa namna anavyoweza.

Wakati ule timu ya Yanga ilipokuwa dhoofu kila mmoja alijua kuwa itakufa nyingi hali ya mshangao mkondo wa kwanza zilienda sare ya bao 2-2 na ule wa pili Simba ikafa 1-0.

Bado haitabiriki ila ni vizuri wakamaliza migogoro yao kabla ya mchezo huo ingekuwa vyema sana kwa upande wao.

Katika msimamo wa ligi Yanga ipo nafasi ya pili wakati samba ikiwa nafasi ya nne na alama zake 13.

MANULA KAKOLANYA KUTIBA SEMBE YA MWARAMI

Walinzi wa goli la mabingwa nchi Simba SC,  Aishi Manula na Beno Kakolanya ndio sababu ya tetesi za kuondolewa kwa kocha wa magolikipa Mwarami Mohamedi.

Kesi hii haikuanza mwaka huu bali tangu msimu uliopita makosa madogomadogo ya udakaji yatapeperusha sembe ya kocha huyo.

Sekeseke lilianzia tangu ile sare ya goli 2-2 ya watani wa jadi kuanzia pale kibarua cha kocha huyo kilikuwa matatani sana na hatimaye huenda  siku si nyingi ikafikia tamati.

Msimu huu makosa ya makipa hao bado yanaonekana waziwazi, goli la Aishi Manula mkoani Sumbawanga walipocheza na Tanzania Prisons limeonekana wazi kuwa kipa hafuati maelezo ya kocha au hajafundishwa kabisa.

Makosa hayo yanaonekana kujirudia kutokana na maoni ya watu mbalimbali hivyo moja ya chanzo ya kuondolewa kwa kocha huyo.

Kakolanya yeye anaonekana hakubaliani na baadhi ya makocha wake maana hata katika mchezo waliopoteza bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting alionekana kusigana na kocha msaidi wa Simba Seleman Matola lakini muendelezo wake sio mzuri.

Makosa yote hayo yamekusanywa na nani atabebeshwa mzigo ni kocha anayehusika na sehemu hiyo na simwingine ni Mwarami Mohamedi.

RWEYEMAMU NAYE AONDOKA NA WENGINE

Simba imemtupia virago aliyekuwa Meneja wa timu Patrick Rweyemamu baada ya kuhudumu katika timu hiyo kwa muda sasa mbio zake zimeisha siku ya Jumanne na sasa sio kiongozi tena wa timu hiyo.

Haya mambo hutokea mara kwa mara pindi inapotokea matatizo viongozi wa juu wanatafuta nani wa kumnyoa upara wakikuta mnyonge basi jumba bovu litakuangukia.

Kwa swala la Rweyemamu  huenda kuna vitu vingi viliendelea ambavyo haviko sawa na wakaamua kumfurusha, hatupingi kwakuwa hatujakuwepo wakati wanafanya uamuzi huo.

Kabla sijaendelea na ujumbe huo nikumbuke tu miongoni mwa Meneja wa timu kubwa Tanzania aliyekuwa anafuata weledi wa hali ya juu hasa katika kuongea na vyombo vya habari.

Hakuwa anaringa anakupa taarifa muda wowote unapoitaka tena kwa ubora ule unaohitajika, hakusumbui ukijitambulisha vizuri unafanya naye mahojiano bila shaka.

Naamini pia hata utendaji kazi wake, ulikuwa wa hali ya juu lakini kila kitu kina mwisho.

KILICHOMUONDOA RWEYEMAMU SIMBA ?

Kila mmoja anaweza kuongea lake lakini tatizo kubwa la Rweyemamu kuondoka Simba ni maelewano baina yake na kocha mkuu Sven Vandenbroeck.

Ilitokea tangu msimu uliopita iliarifiwa kuwa hakuna maelewano kati ya Meneja na kocha na ilibaki kidogo kocha aondoke ila wakayaweka sawa na akaamua kubaki.

Sasa hali mbaya Simba ndio akatafutwa nani atupiwe virago akaanza Meneja.

Iko hivi, viongozi wa Simba walitakiwa wachague moja kuendelea na Meneja au kuendelea na kocha mkuu.

Yaani aondoke Vandenbroeck au Rweyemamu sasa uongozi umeona aanze Meneja kisha wengine watafuata.

Tanzania Sports
ipo kazi kweli kweli….

Baada ya kuona mambo yanazidi kufuka moshi, kinachoelezwa Rweyemamu alikuwa anataka usawa kwa wachezaji hakutaka makundi  wakati huo kocha mkuu yeye akihitalifiana na mchezaji ujue huyo ataozea benchi.

Utetezi wake Rweyeymamu na kuhitaji haki umemfanya aondoke japo kuna mengine ya ndani ya timu ambayo wameyaficha.

WENGINE WALIOTEMWA

Baada ya Jumatatu kutangazwa habari za kufutwa kazi meneja huyo sasa wengine wanne nao wamefukuza.

Baada kuondoka Rweyemamu sasa wakataofuata ni benchi zima la ufundi la timu hiyo , iliwahi kusemekana kuwa kocha msaidizi Selemani Matola hakuwa na maelawano mazuri na kocha mkuu hapo awali hivyo panga hilo litamkuta.

Kwa namna ilivyo unaweza kuona namna gani kocha na jopo lake zima la ufundi halikuwa na maelewano.

Unadhani atabaki mtu hata kama mmoja kashatolewa sadaka? wewe ngoja uone nini kinaenda kutokea.

Baba Chico

Huyu alikuwa katika kitengo cha Habari amefukuzwa kazi lakini pia mwenzake aliyekuwa kitengo hicho aliyefahamika kwa jina la Jacob.

Ieleweke kocha mkuu na kocha msaidizi hawajaondolewa bado ila nao kaa la moto liko kooni muda wowote utasikia kinawaka.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Sven wa Simba Ajiandae Kisaikolojia

Sean Dyche

MAUZO YA KLABU EPL: