in ,

SERENGETI BOYS INAZIDI KUTUPA SABABU YA KUICHANGIA

Hakuna kitu kizuri katika maisha ya mwanadamu kama kupata Mwenzi
sahihi wa maisha yako. Siku zote mwezi sahihi hufanya ndoa kuwa bora
na maisha ya mwanadamu siku zote yanatakiwa yaishie kwenye ndoa maana
ni agizo ambalo mwenyezi Mungu alitupatia.

Kujari siku zote huoneshwa kwa wanaokupenda, na hakuna upendo mkubwa
kama upendo unaojali furaha ya mwanadamu mwenzako, kumfanya mwanadamu
mwenzako awe na furaha muda mwingi wa maisha yake hii ni zawadi kubwa
sana.

Ni wachache sana wanaojua kutengeneza furaha ya wenzao ndiyo maana
asilimia kubwa ya watu hulia kwa maumivu wanayokumbana nayo kwenye
maisha kwa sababu hawajapata watu sahihi wa kuwapatia furaha.

Tumekuwa tukitembea katika maumivu makubwa sana kwa muda mrefu,
hatujawahi kuwa na furaha muda mwingi mwa maisha yetu ya soka.

Vizazi vingi sana vinakuja na kupita, lakini kila vikija na kupita
hutuachia maumivu makubwa kwenye nyoyo zetu. Manung’uniko na
masononeko yamekuwa hayatoki katika mioyo zetu.

Tulipoteza tumaini, hatukuwa tunaiona njia sahihi ya kupita kwa sababu
tulikosa mwanga ambao ungetumika gizani ili tuweze kuona njia ya
kupitia.

Tuliwaamini wengi kutuongoza lakini wakatupitisha katika njia zenye
miba ambayo tuliishiwa kuchomwa na kuambulia maumivu makubwa katika
miguu yetu na hii yote ni kwa sababu hatukuwa na taa ya kutuongoza
kwenye njia yetu ya soka.

Muda huu kichwani kwetu kuna taa yenye mwanga mkali, mwanga ambao
unatupa nafasi kubwa kwetu sisi kuona njia sahihi ya kupita.

Jumamosi wakati Serengeti boys ilipokuwa inacheza na Gabon ambao ni
wenyeji wa mashindano ya Afcon kwa vijana ilituonesha dhahiri kuwa ni
taa sahihi ambayo inatupa mwanga ng’aavu kule tunapoelekea.

Sasa hivi tunapoelekea tunapajua vizuri kwa sababu njia tunayopitia
tunaiona vizuri kwa kuwa tuna mwanga ambao unatumika kutuongoza kutoka
gizani.

Muda mwingi giza lilikuwa limetanda katika mboni zetu na hii ni
kutokana na kutembea kwenye giza muda mrefu bila mwanga wa kutuongoza.

Ujumbe ambao Serengeti boys ulitupa sisi Watanzania ile jumamosi
ilipokuwa inacheza na Gabon ulitosha kutukumbusha kuwa tuna deni kubwa
sana ambalo tunatakiwa tulitimize dhidi ya timu yetu hii ya taifa ya
Vijana.

Hii timu ni yetu sote na sisi tunahusika katika malezi ya hii timu kwa
kiasi kikubwa.

Unaweza ukawa hujaelewa ujumbe walioutoa jumamosi dhidi ya Gabon,
lakini miguu yao ilitueleza wazi kuwa wapo tayari kutupatia furaha
tena katika sokaletu. Maumivu ambayo tumekuwa tukitembea nayo katika
sokaletu wako tayari kuyafuta.

Furaha iliyopotea katika mioyo yetu wapo tayari kuturudishia.
Inawezekana kabisa tukawa tumetumia muda mrefu kutafuta mwenza wetu wa
maisha ambaye ni sahihi lakini wakati huu tumepata mtu ambaye yuko
tayari kutembea na sisi katika hali zote.

Kumpata mtu wa kukupa furaha haitoshi bali unatakiwa uende zaidi ya
hapo na kikubwa unachotakiwa kukifanya ni kumtunza kwa nguvu na hali
zote ili azidi kutimiza jukumu lake kubwa la kukupa furaha.

Hatutakiwi kuwavunja mioyo tena katika hatua hii, tunatakiwa tuzidi
kupigana kadri ya uwezo wetu kuhakikisha hakuna kitu kinachowavunja
mioyo kwa kuwachangia pesa ambazo zitaongeza hali na hamasa kubwa ya
kupigana.

Timu iliyopo inauwezo mkubwa sana wa kutupa furaha tunayoihitaji muda
mrefu katika maisha yetu ya soka, lakini hamasa ndicho kitu ambacho
ƙkinatakiwa kilindwe katika upiganaji wao.

Hivi vita ambayo wapo Serengeti boys ni vita ambayo wapo wa kiitetea
na kuipigania nchi yetu.

Na hii ina maanisha kuwa wanajeshi wetu wako vitani wakiipigania nchi
yetu , tunachotakiwa sisi kutowatupa wanajeshi wetu kwa kuwachangia
pesa ambayo itawasaidia kupigana kwa hali huku morali yao ikiwa juu
sana.

Chochote kidogo ulichonacho nacho kitakuwa kikubwa sana kwa timu yetu
hii kufika mbali.

Tulianzia Tanzania , tupo Gabon, tushirikianeni kwa pamoja kwenda wote India.

Changia kupitia 0687333222. Kuna furaha kubwa sana kwa mtu yoyote kuwa
sehemu ya ushindi wa vita, chukua silaha yako tuwe sehemu ya ushindi
wa vita hii.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

HILI LA MAANDAMANO YA SIMBA WANAFANYA KWENYE TAA NYEKUNDU

Tanzania Sports

Hii ya kadi za njano ni fedheha kwa TFF