in

Samatta Alitakiwa Awe Mbinafsi

Lomana Lualua

Samatta alitakiwa awe mbinafsi ili atengeneze jina lake licha ya kuwekwa katika nafasi isiyokidhi mahitaji yake.

Ni ngumu kuwa mchoyo katika timu yupo Jack Grealish ambaye yeye ndiye mchoyo namba moja, lakini ilitakiwa naye afuate nyayo zake.

Hii inaitwa kujilipua, angefanya hivyo huenda ingesaidia kuona anakaa na mpira na ikiwezekana kufunga magoli.

MS
Mbwana akiwa kwenye ubora wake

Naamani kwa muda aliofika angefunga magoli 5 yangemfanya kocha  Dean Smith asifikirie kuleta watu wengi katika eneo analocheza ndugu yetu.

Kuna baadhi ya nyota wa Kiafrika walipoingia ligi kuu England โ€˜EPLโ€™ walijitahidi kuwa wabinafsi ndio maana walifanikiwa, mfano Lomana Lualua, Yakubu Ayegbeni na  Erick Djemba Djemba hao ni mfano tu waliamua kuwa wabinafsi ili watengeneze maisha yao na kweli waliweza.

Samatta alipokuwa anachezza KRC Genk ni tofuati kabisa na huku Aston Villa, kule alicheza kama mtu wa mwisho kutoa maamuzi anapoliekea goli.

Sasa huku mara yupo pembeni  kidogo yupo kati ilimpa wakati mgumu na kocha kukosa subra kumemfanya atolewe klabuni hapo.

Ametua Fenarbahce ambapo mastaa wengi walipita hapo kama vile Jay Jay Okocha, Robin Van Persie na Robert Carlos.

TUMKARIBISHE UTURUKI SASA

Tanzania Sports
JAY-JAY OKOCHA AT FENERBAHร‡E

Karibu katika ‘Derby’ yenye uhasama Mbwana Samatta, hapa Uturuki kuna desturi yetu ya kucheza kwa bidii maana wakati mpo uwanjani majukwaani wanauwasha moto.

Kama ilivyo kawaida ya Wabongo unapokwenda popote nasie tupo huko huko hadi utakapo amua kuacha mpira, ila ukiona umechoka usijaribu kumalizia mpira bongo heshima yako utaiweka matundu.

Nakupa maelezo mafupi ya mji huu wa Istanbul, mji ambao una starehe nyingi kuliko zile za Dar es Sala unazozifahamu, huku tunakula bata ‘Unlimited’ lakini nakujua wewe uko makini sana na kazi yako.

Samatta utaendelea kuandika historia kila siku na sie tutaziandika kwani uliyoyafanya makubwa kupita maelezo, sasa nakueleza historia ambayo utaiandika hivi karibuni. 

Fenerbahรงe S.K. ipo katika mji wa Instanbul lakini kipande kidogo kipo ambacho kina  makazi ya timu hiyo kipo Bara la Asia lakini sehemu kubwa kabisa na mji huo ipo Ulaya ambayo ndio sehemu kubwa ya Uturuki.

Kitu kimoja nachokuomba waambie kuwa sisi Wabongo tutavamia mitandao yao ya kijamii sababu yako hasa katika Instagram.

Kuna bahari imepita katikati imegawanyisha katika sehemu ya Istanbul ambapo sasa imeunganishwa na daraja, hivyo Galatasalay ambayo nayo ipo katika mji huo ipo huku upande wa pili wa sehemu kubwa ya Uturuki ambapo pembezoni kidogo wapo wabishi Besiktas ambao nao utacheza nao nayo ‘Battle’ ya kufa mtu.

Fenerbahรงe S.K.ni sehemu sahihi kwako kwani msimu ujao utaenda kucheza timu za Italia au Ufaransa ukitupia japo magoli 10.

Ujue umechukuliwa Fenabahce kuziba nafasi ya mchezaji  aliyefunga goli 15 na akapata nafasi ya kusaini timu moja huko Italia.

Kuna wajumbe wamenituma nikwambie uwaulize viongozi wa timu yako mpya kuwa kuna mchezaji mwenye kaliba ya uchoyo kama Jack Grealish, kama yupo watupe jina tuta ‘dealโ€™ naye.

Hizo salamu kutoka kwa wajumbe wa soka bongo, usizichukulie kwa ukubwa huo porojo hizi huwa tunajifariji namna tunavyo kupenda wewe fanya kazi.

Samatta amesaini kandarasi ya miaka 4 kuitumikia Fenerbahรงe S.K.ya Uturuki baada ya kukaa miezi 8 katika timu ya Aston Villa, amefunga magoli 2, moja ligi kuu England lingine katika fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Manchester City.

Walio wengi wanaweza kuongea mengi juu ya uhamisho huo, wengine wakimponda nyota huyo lakini hawajui furaha atakayoleta katika taifa pamoja na maslahi yake binafsi.

UTOFAUTI

Fenabahce inauhakika wa kuchukua ubingwa wa ligi ya Uturuki kuliko Aston Villa kufika ‘Top four’ ligi kuu England hivyo Samatta anauhakika wa kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Uhakika wa kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kila wiki kuliko alipokuwa hapo awali yaani Aston Villa.

Rahisi sana kutoboa kwani bado yupo Ulaya na kuna uwezekano wa kuonesha kipaji chake halisi hivyo akifanya vizuri itakuwa tiketi yake kurudi EPL au kwenda ligi nyingine kubwa kama vile La Liga, Serie A, Liegue 1 na Bundasliga.

SAMATTA AFANYE NINI

Waswahili wanasema kufa kwa Imamu sio mwisho wa ibada,  hivyo basi ‘Samagoal’ anatakiwa aongeze juhudi na apambane kweli ili afikie malengo.

Ni kweli EPL ni ligi bora kabisa lakini kuna ligi nyingine pia  wachezaji wote hawawezi kucheza sehemu moja, huku sasa ndio awaoneshe kuwa yeye ni moto kwa kuonesha kiwango safi kila anapopata nafasi.

Atafute rafiki haraka kama alivyofanya kwa Nakamba ambaye ni Mzimbabwe, ili asijihisi yuko mpweke sana, ajenge urafiki na kocha, urafiki huo ni kufanya vizuri mazoezini na uwanjani.

Safari ya Samatta sasa imefika tamati kucheza EPL nahii imetokana na kutopata nafasi ya kuonesha uwezo wako.

Wajumbe unaohoji juu ya uwezo wake eleweni tu kuwa ndugu yetu bado yupo Ulaya na anauwezo wa kurudi EPL akiwa na timu nyingine.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mbwana Samatta

Wachezaji wa Tanzania watafute โ€˜Connectionโ€™

Yanga

Azam Imara Kuliko Yanga Na Simba