in , , ,

Safari ya Cole inafika mwisho Chelsea?

*Vidic naye adaiwa kuaga Manchester United

Beki wa kushoto aliyepata kudaiwa kuwa bora zaidi duniani, Ashley Cole anakaribia kuondoka Chelsea.
Mchezaji huyo aliyeichezea England mechi 98 tayari anawindwa na klabu tatu kubwa.
Mkataba wa Cole unaisha mwisho wa msimu huu, ambapo inadaiwa kwamba amepewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja tu asioutaka, kama ilivyokuwa kwa Didier Drogba.
Sera ya Chelsea imekuwa kwamba hakuna kutoa mkataba wa zaidi ya mwaka kwa wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 30, na Cole anayo 31.
Habari hizi zinakuja wakati beki huyo akiomba huruma ya Chama cha Soka (FA) England baada ya kuwatukana maofisa wake kwa kutumia mtandao jamii.
Cole alikasirishwa na jinsi FA kubeza utetezi wake kwa John Terry aliyemtusi kibaguzi Antony Ferdinand wa Queen Park Rangers (QPR). FA ilisema Cole ni mwongo na ushahidi wa Terry ulikuwa wa kutunga.
Wakati safari ya Cole ikikaribia ukingoni Stamford Bridge kama Drogba anayecheza China, makocha wake wa zamani, Jose Mournho wa Real Madrid na Carlo Ancelotti wa Paris Saint-Germain wanadaiwa kusubiri kumchukua.
Ni Ancelotti aliyetangaza hivi karibuni kwamba Cole ndiye beki bora zaidi wa kushoto, na kwamba klabu inayotaka uimara lazima imtafute.
Hata hivyo, si ajabu Cole asiondoke kwenye Ligi Kuu, kwani Kocha Mkuu wa Manchester United, Alex Ferguson anadaiwa kumtaka Cole siku nyingi.
Kama alivyomnyakua Robin Van Persie wa Arsenal mkataba wake ulipokaribia kumalizika Emirates, Ferguson anaelekea kunyatia mazingira ya Chelsea na Cole ili Januari aingie Old Trafford.
Lakini, kwa upande mwingine inadaiwa kwamba Cole anatikisa tu kiberiti wala hana mpango wa kuondoka, bali ni namna ya kupata mkataba mrefu au fedha nyingi zaidi Stamford Bridge.
Watu wa karibu naye wanasema kwamba Chelsea wanatakiwa kuonesha heshima kwa Cole kwa mchango aliotoa kwa timu hadi kutwaa kombe la Ulaya, kwani umri haujamzuia kucheza vyema.
Iwapo Cole ataamua kuondoka Chelsea kwa sababu zozote, kuna uwezekano wa nafasi yake kuchukuliwa na Benoît Assou-Ekotto wa Tottenham Hotspurs.
Taarifa zaidi kuhusu kuhama wachezaji zinamgusa nahodha wa Mashetani Wekundu, Nemnaja Vidic anayehusishwa na kuhamia klabu ya Kirusi inayomwaga noti, Anzhi Makhachkala, inayotaka kumpa mshahara wa Pauni milioni 12 kwa mwaka baada ya kodi.
Hata hivyo, si rahisi kwa Ferguson na United kwa ujumla kumwacha beki huyo wa Serbia aliyerejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu aondoke, kwani ni nguzo kubwa ya safu yao ya ulinzi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TAVA HOLDS ANOTHER COURSE IN MWANZA