in , , ,

Rooney: Man United hapakaliki

*Liverpool yamuuza Downing West Ham
*West Brom yapata mshambuliaji mpya

 

Mshambuliaji nguli wa Manchester United, Wayne Rooney ametoboa siri kwamba hatarajii kubaki Old Trafford, kwa sababu hapakaliki.
Rooney ameshaomba kuondoka zaidi ya mara mbili, lakini kocha wa awali Alex Ferguson na huyu wa sasa, David Moyes wamemkatalia, na bado wanamchunia kumhakikishia nafasi kikosi cha kwanza.
Rooney kwa sasa ana raha sana, kwa vile yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kinachojiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Scotland, na amemshukuru kocha Roy Hodgson kwa kumwamini na kumjali.
Rooney amemweleza Nahodha wa England, Steven Gerrard juu ya sintofahamu iliyopo Old Trafford, ambapo katika mechi zote za maandalizi ya ligi alicheza moja tu kwa madai ya ugonjwa, lakini anasema yu tayari kuliwakilisha taifa lake Jumatano hii.
Gerrard akizungumza kabla ya mechi baina ya mataifa hayo mawili yaliyokutana mara ya mwisho 1999, alisema Rooney alimmegea siri kwamba hadhani ataweza tena kukaa Manchester United.
Moyes, bosi wake wa zamani Everton, amemwambia wazi kwamba hatakiwi kuondoka hadi mkataba wake uishe na kwamba atakuwa chaguo la pili kwenye ushambuliaji baada ya Robin van Persie.
Rooney (27) anatakiwa na Chelsea na Arsenal, lakini Man U wamekataa kumuuza, kama ambavyo wenyewe wamekataliwa kumnunua Cesc Fabregas wa Barcelona.
Makocha wengi wa klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) inayoanza Jumapili hii, wanataka ama wachezaji wao wasitumike, wacheze dakika chache au wakicheza mechi nzima warejee wakiwa fiti kwa ajili ya ligi.

 

WEST HAM YATWAA WINGA WA LIVERPOOL

KLABU YA West Ham United imemsajili winga wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Stewart Downing kwa ada ya pauni milioni tano.
Downing (29) amesaini mkataba wa miaka minne Upton Park chini ya kocha Sam Allardyce na anamfuata mpachika mabao aliyekuwa Anfield, Andy Carroll ambaye baada ya muda wake wa mkopo, amesajili moja kwa moja.
Downing alisajiliwa Liverpool kwa gharama ya pauni milioni 20 kutoka Aston Villa mwaka 2011. Kocha Brendan Rodgers amekuwa akimchagiza Downing aliyesajiliwa na kocha mtangulizi, Kenny Dalglish, akiwa hafurahishwi na aina ya uchezaji wake, ambapo alikuwa akimbadilisha namba mara kwa mara, na sasa ameamua kumtua.
Carroll pia alisajiliwa na Dalglish kwa thamani ya pauni milioni 35 Januari 2011, lakini hakuonesha makali yaliyotarajiwa, na Rodgers ndiye alimtoa kwa mkopo West Ham na sasa amemuuza kabisa kwa pauni milioni 15.

 

WEST BROM NA PENGO LA LUKAKU

Wayne Rooney of Manchester United vs Everton. ...
Wayne Rooney of Manchester United vs Everton. at Old Trafford, Manchester. (Photo credit: Wikipedia)

Kocha wa West Bromwich Albion, Steve Clarke anaelekea kukiimarisha kikosi chake baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku wa Chelsea aliyekuwa hapo kwa mkopo.
Clarke amekamilisha mpango wa kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Udinese, Matej Vydra anayetarajiwa kuwa hapo Hawthorns kwa msimu mzima.
Vydra (21) alifnga mabao 20 alipokuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Watford msimu uliopita na kuwasaidia kushika nafasi ya tatu kwenye Championship, ligi iliyo ngazi moja chini ya EPL.
“Alifanya vizuri sana akiwa na Watford, tunaamini kwamba ana viwango vinavyotakiwa katika kupachika mabao kwenye ligi kubwa,” Clarke akasema.
Mchezaji huyo ni raia wa Jamhuri ya Czech na anachezea timu ya taifa hilo na mwaka jana alikuwa mchezaji bora wa mwaka katika Championship na anakuwa wa nne kusajiliwa na West Brom msimu huu.
Wengine waliosajiliwa tayari ni mpachika mabao wa Ufaransa aliyechezea timu nyingi, Nicolas Anelka kutoka Juventus, mlinzi Diego Lugano kutoka Paris St-Germain, wote wakiwa ni wachezaji huru.
Mwingine aliyesajiliwa Julai ni beki kutoka Bulgaria, Goran Popov aliyekuwa hapo kwa mkopo kutoka Dynamo Kiev.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

KAMATI KUTANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF

UCHAGUZI TFF KUFANYIKA OKTOBA 18, 2013