in ,

Ronaldo, Messi wanatudai?

CR

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamedumu katika soka la ushindani zaidi ya miaka 15 kwa viwango vya hali ya juu wakitengeneza rekodi nyingi za kuvutia.

Rekodi walizotengeneza kuvunjwa kwake inawezekana ikapita miaka mingi au hata karne kutokana na ugumu wa lgi na mabadiliko ya sheria za soka.

Tuanzie hapa kwanza, dalili inaonesha wachezaji hao jua lishaanza kuzama kulingana na umri wao ikiwa Ronaldo amefikisha miaka 35 huku Messi akiwa na 33.

Dalili nyingi zinaonesha kweli wameshachoka hadi kufikia kuelekeaa mwishoni mwa msimu katika ligi wanazo shiriki huwa wanafikisha zaidi ya mabao 30, ila msimu huu tofauti kwanini Ronaldo ana magoli 28 wakati Messi ana magoli 22.

Hizo zote ni dalili za mambo kwenda mrama yaani waswahili husema ‘mbio za ukingoni huishia sakafuni’ au wengine huenda mbali zaidi wanasema  hakuna marefu yasiyo na ncha.

Tanzania Sports
Mtaalamu Messi, akiwa kazini

Ukweli ni kwamba jamaa wamechoka sasa na ni wakati wa vijana kuwapa nafasi ya kuwika, swali la kujiuliza ni kweli wanaweza kudumu katika ubora  kwa miaka 15 na ziada?

Pia wanaweza kufunga magoli zaidi ya 40 kwa msimu mmoja ? Maswali haya kila mmoja anaweza kuyajibu kwa wakati wake kutokana na ugumu wake.

Je wanaweza kufunga magoli matatu kwa mechi moja ‘Hat-trick’ mara nane au kumi kwamsimu ? haya maswali tuwaachie kina Mbappe ambao wanatabiriwa makubwa mbele yao.

Kitu kigumu kabisa kwa vijana wanaochipukia wanaweza kufunga magoli 700 na zaidi katika maisha yao? ambapo tayari Messi na Ronaldo wameshafanya hivyo tayari.

Tukiendelea kuuliza maswali tutawapa presha kubwa vijana wanaohitaji kuchukua nafasi zao kikubwa tuwaache wafanye wanayoyaweza tena wasithubutu kujifananisha na watu hawa wawili.

Tumeshawahi kuona Mreno Luis Nani aliwahi kufananishwa na Ronaldo mwisho wa siku tumeona wapi alipoishia.

Kwa sasa wachezaji hawa wawili wanatudai sisi watoa habari lakini pia hata mashabiki wanaobishana kijiweni.

Huu ndio wakati sahihi wa kusema makubwa waliyoyafanya tusisubiri wakistaafu kisha wanaokuja kuchukuab nafasi zao kama hawafanyi vizuri ndio tuanze kuwakumbuka.

Wale wenzetu waliokuwa miaka ya tisini kweusi mnaona wanavyowapigania wachezaji wao wa wakati huo yaani Pele na Maradona wanawasema vizuri sana tena ikifika wakati ukiwaambia juu ya Ronaldo na Messi wanakwambia hawajafika ubora wa Pele na Maradona.

Japo hata magoli yao tunaambiwa mechi za kirafiki yanachanganywa pia katika rekodi ya ufungaji bora ila sie tunachuna tu kwakuwa hawa wachezaji wetu tunaona makubwa wanayoyafanya tena kwa ushahidi.

Tuachane na hayo wote tunaamini Pele na Maradona walikuwa bora ila sio bora kama Messi na Ronaldo kwa maoni yangu.

Nina hoja nitakuja kuisema siku moja na nitatoa takwimu zao wakati wa zamani wakina Pele na  wa sasa wa Messi na Ronaldo.

Ronaldo wakati anatoka Sporting Lisbon ya nchini Ureno ile kasi yake pamoja na ubora wa kupiga chenga huku akikata mikasi  katika mguu wake hakuna aliyekuwa mbishi juu ya ubora wake.

Messi anakusanya kijiji anamuangusha Boateng wa Bayern Munich anaenda kufunga goli ikiwa na msimu wa mabeki wenye roho mbaya we unafikira nini hapa.

Mimi binafsi nafurahi kuwa katika kizazi hiki ambacho kina Ronaldo na Messi nikianagalia ubora uliotukuka.

Japo tukirudi katika ubora kati yao kuna makundi mawili wengine Messi huku upande wa pili Ronaldo, sio kwa bahati mbaya bali ubora wao ndio umefanya watu wagawanyike na kuwa pande mbili ila ukiongelea ubora hawa watu noma sana.

Ronaldo alichokosa ni kombe la dunia pekee katika maisha ya mpira huku akichukua makombe yote unayoyajua wewe katika soka la ushindani.

Tuhesabu kwa pamoja, England amechukua kombe la FA, EPL, Carling pamoja na UEFA.

Hali kadhalika kule Hispania akiwana Real Madrid amechukua yote ya kule.

Makombe ya UEFA kachukua yote akiwa katika ngazi yaklabu huku kwa timu ya taifa amechukua kombe la Ulaya kwa mataifa ya huko.

Upande wa pili Lionel Messi amechukua makombe yote ya nchini Hispania na UEFA huku akitengeneza rekodi za aina yake  ambazo kuzivunja itachukua muda.

Alichokosa kombe la taifa lake Argentina na lile la Dunia hapa unaweza kuona namna gani watu hawa wanavipaji vya aina yake.

Tena ukitaka kuzungunzia ushindani hata katika maisha ya kawaida Messi ana watoto wane wakati Ronaldo akiwa na wanne.

Tuzo binafasi hawa watu hawajapishana sana kwani katika ile ya Ballon d’or Messi ana sita Ronaldo tano, wewe unasemaji juu ya watu hawa.

Unaweza kuandika maoni yako chini hapo nawe utoe mchango wako juu ya Messi na Roanldo.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. Asante sana kwa uchambuzi wako. Messi na Ronaldo wamekuwa mahiri sana kwa miaka ya hivi karibuni. Ila naona tusimsahau mtu aitwaye Ronaldinho. Huyu alikuwa mchaei. Angetulia angefanya makubwa zaidi ya Messi na Ronaldinho. Dinho alikuwa na kipaji matata ambacho kwangu mima nafikiri Messi na Ronaldo hawakuwa nacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
kikosi cha yanga

Yanga Kusajili Wachezaji Tisa

Morrison

Ipo nafasi ya Morrison Simba?