in , , , ,

Ronaldo: Marefa wanatunyonga

Mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo amesema kwamba marefa hawawatendei haki kila wanapokutana na wapinzani wao wa jadi, Barcelona.

Ametoa kauli hiyo baada ya Real Madrid kufungwa 4-3 na mabingwa hao wa Hispania kwenye mechi ya kukata na shoka Jumapili hii.

Ronaldo anasema kwamba haielezeki jinsi maamuzi mabaya yanavyotolewa na waamuzi kwenye mechi baina yao, ambapo Jumapili hii Real Madrid walikuwa wamejiamini sana kwamba wangeshinda kutokana na rekodi yao ya hivi karibuni.

Katika mechi hiyo, mwamuzi Alberto Undiano Mallenco alitoa penati tatu lakini pia alimyoa nje kwa kadi nyekundu mchezaji Sergio Ramos wa Real Madrid katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu.

Lionel Messi alitupia mabao mawili kwa penati tata kama sehemu ya hat-trick yake, ambapo Barca walitoka kusinzia 3-2 na kuwalaza Madrid 4-3 na kufufua upya ndoto zao za ubingwa.

“Ni ngumu sana kwa sababu watu wengi hawakutaka tushinde kwa vile kwa kufanya hivyo Barcelona wangekuwa wametupwa nje ya kinyang’anyiro cha ubingwa wa Hispania. Labda hawataki tuchukue kombe hili,” alisema Ronaldo.

Mreno huyo mwenyewe alifunga bao kwa penati tata pia baada ya Dani Alves kumwangusha nje ya boksi la penati. Ramos alipotolewa nje kwa kumpiga kwanja Neymar kwenye mstari wa boksi, wageni waliona kwamba wakati wao wa kujidai ulifika, na kweli Messi akasawazisha kwa penati.

Barca ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya saba kupitia kwa Andres Iniesta lakini likasawazishwa na Karim Benzema dakika ya 24 kabla Mfaransa huyo huyo hajaongeza jingine dakika ya 24.

Hata hivyo, penati aliyotumbukiza kwenye kwamba Messi ilikuja dakika ya 42 kabla ya hasimu wake, Ronaldo kufunga yake dakika ya 55. Dakika 10 baadaye Messi alifunga tena kwa penati dakika ya 65 kabla ya kufumania nyavu dakika sita kabla ya mechi kumalizika.

“Tunasikitika sana kwa matokeo haya, kwa sababu ukweli ni kwamba tulitakiwa tushinde sisi,” akasema Ronaldo ambaye wakati wa mechi alifika mahali akamfuata mwamuzi kumlalamikia.

Matokeo hayo yanawafanya Atletico Madrid kuongoza ligi kwa kufikisha pointi 70 sawa na Real, huku wakifuatiwa na Barca wenye pointi moja pungufu na Athletic Bilbao wenye pointi 55.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Simba hoi Taifa

Kutoka TFF Leo…..