in , , ,

Riadha amkeni, kwa hili serikali haina lawama – Evarist Chahali

*Vyama vya michezo inabidi viwe vibunifu.

*Mazingira ya Nchi yanaruhusu wanamichezo kufanya vizuri.

 

Kwa siku kadhaa sasa, mjadala ambao unatawala miongoni mwa Watanzania wengi ni matokeo mabaya ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka jana, ambapo zaidi ya asilimia 60 ya watahiniwa wamefeli.

Na kama ilivyo kwa masuala mengi yasipendeza yanayoligusa taifa, serikali imejikuta lawamani tena.Yayumkinika kuhitimisha kuwa kama kuna taasisi ambayo inabebwa lawama nyingi huko nyumbani basi ni serikali yetu.

Linapokuja suala la ufisadi, lawama huelekezwa kwa serikali.Ikiwa ni tatizo sugu la mgao wa umeme, lawama zinaelekezwa kwa serikali. Kadhalika, hali ngumu ya maisha, lawama pia zaelekezwa kwa serikali.

Wakati mwingine lawama hizo huiweka serikali na chama tawala kama kundi moja, pengine kutokana na ukweli kwamba serikali iliyopo madarakani imetokana na ushindi wa CCM kwenye chaguzi zilizopita.

Lazima nikiri kuwa binafsi ni miongoni mwa hao wanaozilaumu serikali mara kwa mara.Lakini kila ninapoilaumu serikali huwa ninahakikisha kuwa lawama hizo si kwa minajili ya kulaumu tu, au kuichukia, bali zinastahili kuelekezwa huko.

Hata hivyo sio kila pungufu linaloikabili Tanzania yetu wa kulaumiwa ni serikali.Na moja ya maeneo ambayo pengine hatustahili kuilaumu serikali yetu ni kusuasua kwetu katika mchezo wa riadha.

Nilianza kupenda riadha tangu nikiwa shule ya msingi (sababu ya msingi ikiwa ni mwalimu wa michezo kutambua kuwa sina sifa stahili za kuingizwa kwenye timu ya soka ya shule). Baada ya kutambua kuwa uwezo wangu kisoka ni mdogo nikadhani labda Ningeweza kutamba kwenye riadha.Well, huko nako ‘nilichemsha’ kwani sikuwa na kasi.

“5,000 m race”. Track and field athletics. The...
“5,000 m race”. Track and field athletics. The 22nd Summer Olympic Games in Moscow (July 19 – August 3, 1980). Athlets: 649 – Suleiman Nyambui (Tanzania) 191 – Miruts Yifter (Ethiopia) 208 – Kaarlo Maaninka (Finland) (Photo credit: Wikipedia)

Lakini pamoja na kutofanikiwa kwangu katika mchezo huo, niliweza kufarijiwa na uwakilishi wa baadhi ya wanariadha wetu mahiri wa enzi hizo,kwa mfano Suleiman Nyambui, Juma Ikangaa, Mwinga Mwanjala, Gidamis Shahanga na Filbert Bayi. Wanamichezo hawa walifanikiwa sana kuitangaza Tanzania yetu kimataifa kupitia mchezo wa riadha.

Majuzi kulikuwa na mashindano ya riadha ya kimataifa hapa Glasgow lakini kama ilivyo kwa mashindano mengi, hakukuwa na Mtanzania hata mmoja. Lakini kilichoniumiza zaidi ni matokeo yetu mabaya kwenye michuano iliyopita ya Olimpiki ambayo ilifanyika hapa Uingereza.

Japo kiujumla nchi yetu imekuwa ikisuasua kwenye michezo mingi, kwenye riadha kusuasua huko kunaambatana na ukweli kuwa huko nyuma tulikuwa katika nafasi nzuri.

Kuna wanaozilaumu serikali kutokana na mwenendo wetu mbaya kwenye riadha, pengine kwa vile-kama nilivyoandika hapo juu- serikali imekuwa ni kama ‘mlengwa mzoefu’ wa lawama mbalimbali, lakini pia yawezekana lawama hizo zinatokana na hisia kwamba serikali ina uwezo wa kuingilia kati na sio tu kuuokoa mchezo huo bali kuturejesha kwenye ramani ya kimataifa kama ilivyokuwa enzi za kina Nyambui na Bayi.

Labda badala ya kuhangaika na nani wa kulaumiwa, tujiulize kwanini tumefika hapa tulipo sasa. Ninatambua kuna sababu mbalimbali,lakini kuu kwangu ni uongozi mbovu wa chama vya riadha (RT) na Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC).

Pasi kuuma maneno, taasisi hizi mbili zimekuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo ya riadha, na michezo mingine kwa upande wa TOC.

Kinachokera zaidi ni ukweli kwamba baadhi ya viongozi wa taasisi hizo ni walewale ambao huko nyuma walituwakilisha vizuri kabisa.Sasa iweje baada ya kuwa viongozi wa taasisi zinazoshughulikia mchezo walioupenda na kuumudu hali inazidi kuwa mbaya?Jibu rahisi ni UBINAFSI.

Yayumkinika kuhisi kuwa wengi wa wanariadha hao wa zamani waligombea nafasi za uongozi huko RT na TOC si kwa minajili ya kuendeleza historia zao za mafanikio bali kujinufaisha wao wenyewe.

Kwalugha nyepesi, waungwana hao wanakabiliwa na tatizo la uzalendo.Haiwaumizi kuona riadha ikisuasua na rekodi walizoweka huko nyuma zikivunjwa na wanariadha wa nchi nyingine bali kwa cha muhimu ni maslahi yao binafsi.

Uzalendo si tatizo kwenye riadha pekee bali binafsi ninaliona tatizo hilo kuwa ni kikwazo kwenye maeneo mengine mengi,na kimsingi theory yangu kuhusu matatizo mbalimbali yanayotukabili kama nchi ni hiyohiyo ya uhaba wa uzalendo.

Tufanyeje? Ninaamini tuna wazalendo kadhaa ambao kwa sababu moja au nyingine hawataki kujihusisha na maeneo mbalimbali yanayokwenda ndivyo sivyo. Lakini hata kama wangekuwa tayari kujihusisha nayo,wanaweza kukumbana na kikwazo cha chaguzi zilizotawaliwa na rushwa ambapo kigezo kikuu cha mgombea kushinda ni uwezo wake wa kuhonga wapiga kura.

Baadhi yetu Tumekuwa tukipiga kelele miaka nenda miaka rudi (na wakati mwingine tukajikuta tukiingia matatizoni). Lakini giving up is not an option. Ni muhimu kwa kila mwenye uchungu na nchi yetu,iwe ni kwenye michezo, siasa,nk asikate tamaa bali kutumia nafasi yake vizuri, iwe kwa kupiga kelele au ikiwezekana kugombea nafasi za uongozi ili uzalendo wao uweze kutafsiriwa kwa vitendo.

Nimalizie makala hii kwa kutoa wito kwa wadau wa riadha na Watanzania kwa ujumla kwamba ifike mahala tuone aibu kuwa wasindikizaji tu.Zifanyikie jitihada za makusudi za kuturejesha kwenye zama zile tulipokuwa miongoni mwa mataifa yanayoweka katika mchezo huo. Kwa upande wa serikali, ili kukwepa lawama zinazokwepeka, ni muhimu ijaribu kuhakikisha kuwa wababaishaji hawapewi fursa ya kuongoza taasisi zinazohusiana na mchezo huo.

Inawezekana, timiza wajibu wako.

[email protected]

C.E.O/ Founder Tanza-Caledonian

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal kwishnei

Man City washinda kwa mbinde