in

Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika zazipagaisha Simba na Yanga

RATIBA ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF)  imezipagaisha timu za Simba na Yanga zitakazoshiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Februari mwakani.
Klabu ya Simba imepanga kumenyana na timu ya Kiyovu  ya Rwanda  wakati Yanga itamenyana na Klabu Kongwe Afrika ya Zamalek kutoka Misri katika michezo itakayofanyika katikati ya Februari mwakani.


Timu za Yanga na Simba zimeonekana kuhaha zaidi wiki hii baada ya ratiba kutangazwa ili hali kwa miezi kadhaa zilijua kwamba michuano ya aina hiyo itakuwapo, lakini hazikuwa na mipango ya kuziimarisha timu zao.
Yanga ndiyo iliyozidiwa zaidi kwani, mara baada ya ratiba kutangazwa,  kocha mkuu wa timu hiyo Kostadin  Papic alitangaza wazi kwamba mechi hiyo ni pasua kichwa kwake.
Papic alisema atatangaza programu akisisitiza kwamba  kama itafuatwa itasaidia kuijenga timu hiyo kwa kuikabili Zamalek ambayo kwa miaka mingi imekuwa tishio kwa timu za Tanzania hususan Yanga.
Katika kile kinachoonekana kwamba ni kuitikia mipango ya kocha huyo, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Lyoyd Nchunga wiki hii alitangaza kwamba timu yake inatarajia kwenda Afrika Kusini kuweka kambi huku akisisitiza kwamba pia itacheza mechi za majaribio.
Miongoni mwa timu alizozitaja kutaka kucheza nazo kabla ya kuwavaa mafarao wa Misri ni Sofapaka ya Kenya na ile ya Mamlaka ya mapato Uganda (URA)  ambazo pia zina upinzani mkali nchini mwao.
Wakati Yanga ikiwa na mipango hiyo, naye Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage alitangaza  kwamba watazitumia mechi za Ligi Kuu mzunguko wa pili zitakazoanza Januari kujinoa kwa ajili ya kupambana na Kiyovu.
Lakini pia baada ya siku mbili kupita, kiongozi huyo alisema timu yake sasa inatarajia kwenda nchini Malawi kwa ajili ya kambi ambako itapambana na klabu kadhaa za huko.
Rage alisema timu ya Kiyovu alishaiona na kwamba ni ngumu sana kiasi kwamba kwa sasa inamnyima usingizi.
Hatua zote hizo zinachukuliwa na viongozi wa klabu kubwa hizo kama dharura wakati ukweli ni kwamba  walijua kuwapo kwa michuano hiyo tangu waliposhika nafasi ya kwanza na ya pili mwaka jana.
Baadhi ya wapenzi wa soka nchini walikosoa  maandalizi ya papara  wanayofanya viongozi wa klabu hizo wakisema  walichotakiwa ni kuwaweka wachezaji katika mazingira ya kucheza michuano ya kimataifa  tangu mwanzo.
“Maandalizi ya zimamoto ndiyo yanayoziua timu za Tanzania”, alisema mwanamichezo maarufu na shabiki wa Man U, aliyejitambusha kwa jina la Brighton Mwakasumbula.
Alisema kwa kawaida viongozi wa timu hizo walitakiwa kuwa na programu  mbili  ambazo ni ile ya ligi kuu na nyingine ya michuano ya kimataifa  tangu walipopata tiketi ya kushiriki michuano mikubwa Afrika.
Lakini baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walisema   pamoja na kuchelewa kwa maandalizi, wana imani timu zao zitafanya vizuri.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chalenji yaacha madeni – TFF

Outing with friends in London..