in

Ramos ‘beki mshambuliaji’ na rekodi La Liga

Sergio Ramos

UTANI wa mashabiki unaweza kuibua msisimko au hasira. Wenye hasira ni wale ambao timu zao zinafanya vibaya au kufungwa mechi fulani. Awali wapo mashabiki wa timu pinzani wanawatania wale wa Real Madrid kuwa timu hiyo haina mashambuliaji mwenye uwezo mkubwa, matokeo yake timu imekuwa ikimtegemea beki wa kati Sergio Ramos.

Ili kudhihirisha utani wao, baada ya kutwaa La Liga wanasema Sergio Ramos ni ‘beki mshambuliaji’ ambaye amefunga mabao muhimu kuliko washambuliaji wa Real Madrid akina Karim Benzema, Gareth Bale, Lucas Vazquez, Mariano Diaz na Luka Jovic. Pamoja na utani huo kuwa Ramos amekuwa beki mshambuliaji aliyefungia mabao mengi timu yake lakini ukweli ni kwamba amekuwa akifunga kwa miaka mingi.

KUVUNJA REKODI YA GETAFE

Taji la La Liga kwa Real Madrid msimu huu limekuja kwa aina yake. kwanza ineleweka hakuna sherehe. Lakini pili Sergio Ramos amevunja rekodi iliyodumu kwa miaka 15 iliyopita. Ramos alivunja rekodi hiyo katika pambano lao la mwisho dhidi ya Leganes ambao sare ya 2-2 haikuweza kuwaokoa kushuka daraja. Msimu ujao Laganes watacheza ligi daraja la kwanza.

Ramos alifunga bao la 11 la Ligi Kuu Hispania dhidi ya Leganes, ambalo lilimfanya awe beki wa akwanza kufanya hivyo tagu kuanza kwa karne ya 21. Beki mahiri Mariano Pernia aliweka rekodi ya kufunga mabao 10 ambayo ni mengi tangu kuanza karne ya 21 kwa mchezaji wa nafasi yake. rekodi ya Mariano Pernia iliwekwa miaka 15 iliyopita.

Tangu iliporejea La Liga mwezi Juni hadi ilipohitimishwa, Ramos alifunga mabao mengi kama Lionel Messi aliyepachika mabao 6, hivyo akawa chachu ya mafanikio ya Real Madrid msimu huu.

 ‘IMPORTANTISIMO’

Kwa lugha yetu ya Kiswahili  tunasema nahodha au kapteni wa timu. Wahispania wanasema El Capitano. Neno ‘Importantisimo’ kwa lugha ya Kiswahili tunasema ‘muhimu sana au kitu muhimu’. Wahispania wanasema, “Importantisimo” kuonyesha umuhimu wa mtu.

Wakati fulani Lucas Vazquez aliliambia gazeti la Marca kuwa Real Madrid ina kiongozi thabiti ambaye anapendwa na wachezaji wote ndani na nje ya uwanja. Hakuna supastaa pale Madrid mwenye ubavu wa kubishana na Ramos.

Lucas Vazquez huwa anasema “tumetulia uwanjani kwa sababu yuko bosi wetu, kila kitu ni safi,”. Vazquez alikuwa akimaanisha Ramos. Ramos ni ‘Importantisimo’.

Pengine sasa kwa kuvunja rekodi hii inaonesha wazi kuwa Ramos ni mchezaji wa daraja kubwa zaidi. Ametoka katika nafasi yake ya beki wa kati hadi kupika mabao na kufunga. Bila shaka hii ndiyo siri ya Real Madrid leo.

Mafanikio ya Zinedine Zidane tangu alipochukua ukocha wa Real Madrid, yameegemea kwenye uti wa mgongo unaoundwa na Sergio Ramos. Ingawaje Ronaldo aliamua kuhama lakini Ramos amekiongoza vema kikosi cha Real Madrid na kuhakikisha kinaleta mafanikio. Ramos amepitia vipindi vingi vya kupanda na kushuka kwa timu, lakini amesimama imara. Na sasa umri unamtupa mkono, lakini amekuwa chachu ya kupachika mabao na kuhakikisha Real Madrid inabaki kuwa imara wakati wote.

Umuhimu wa beki huyu ni sababu tosha ya kumsikia Lucas Vazquez akisistiza kuwa utulivu wa wachezaji klabuni ni kwa sababu ya uongozi wa kapteni wao. Sergio Ramos alijiunga Real Madrid akiwa na miaka 19 akitokea kwenye klabu ya nyumbani kwao Sevilla.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Kocha wa Yanga

Luc Aymael kajinyima ajira mwenyewe

Uwanja wa Mkapa

Nani Kufunga Goli Uwanja Wa Mkapa ?