in

Raha na kadhia UCL

UEFA

Hatimaye Ufaransa na Ujerumani zimeibuka videdea katika ngazi ya klabu, baada ya Lyon na Paris Saint-Germain (PSG) kwa upande mmoja na Bayern Munich na RB Leipzig upande mwingine kufuzu kwa fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Zilikuwa robo fainali za aina yake, ambapo Bayern waliushangaza ulimwengu wa soka kwa kuwachakaza Barcelona mabao 8-2 kabla ya Lyon kuwachapa Manchester City 3-1, mechi zote zikifanyika jijini Lisbon, Ureno na ni kwa mkondo mmoja kutokana na janga la Covid-19.

Hii ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2012/13 kwa mataifa mawili tu kutoa timu zote nne za kucheza nusu fainali. Matokeo haya yamekuwa kama udhalilishaji kwa Barcelona huku Man City waliokuwa wanatarajia wabebe kombe wakiachwa kwa msimu wa tatu mfululizo wakiishia robo fainali.

Kocha Pep Guardiola alionesha wazi mshangao na masikitiko yake, akisema Lyon walicheza vyema kuwapita, akakiri kwamba yeye na timu yake bado wamedhihirisha hawajaweza kuvuka robo fainali, akaahidi kwamba watajaribu wakati mwingine, akiwa kama mtu aliyekata tamaa.

Tanzania Sports
UEFA

Guardiola ameonekana kuwa na uhuru mkubwa na kujiamini kwingi, lakini matajiri wa Etihad wamekuwa wakitaka watawale Ulaya kwa kutwaa taji hilo, wakiona kwamba ubingwa ndani ya England hautoshi kwa jinsi wanavyomwaga fedha nyingi kununua wachezaji nyota na ghali.

Kwenye robo fainali hii, Guardiola aliamua kuchezesha kwa mtindo wa kuwa kana kwamba wanawafunga Kamba wapinzani wao pale nyuma, akiwaanzisha benchi Bernardo, David Silva, Riyad Mahrez na Phil Foden wakianzia benchi.

Ni miaka mitatu tofauti lakini wameishia hatua ile ile, wakishindwa mara ya kwanza ambapo ingesemwa kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa, na wao wameshindwa mara ya tatu, ikionesha kwamba bado Guardiola hajapata formula maridhawa ya kuvuka kihunzi hicho.

Hawakucheza vibaya sana, kwa sababu walitumia nidhamu japo wakatangulia kufungwa kabla ya kusawazisha, kisha wakafungwa bao tata, kwani mfungaji alionekana kwamba alicheza rafu kabla ya kutikisa nyavu. 

Wakati Manchester City wakijikusanya wasawazishe ilikuwa mshangao kwa Raheem Sterling kupiga mpira juu akiwa na lango peke yake na wakati wakitafakari na kujipaga wakafyatuliwa ten ana ikawa ndio msumari wa mwisho kwenye jeneza lao.

Watu wengi wa soka waliona kwamba kwa kocha wa aina ya Guardiola, aliyefanya vyema ndani na nje ya nchi akiwa na Barcelona na Bayern Munich, pia kwa aina ya wachezaji alio nao, basi wangevuka hatua hii lakini haikuwa.

Ilikuwa ni katika dimba la Estádio José Alvalade, ambako kwa mara nyingine Guardiola aliendeleza urembaji wa gemu, akijua kwamba ni mechi ya mtoano hivyo ilitakiwa wacheze kwa shinikizo ili wapate mabao ya haraka. Na ni kwa mfumo wake anaotaka kufurahisha wanaotazama, ilikuwa ni pasi, kurudi nyuma pasipo kutia presha ipasavyo lango la wapinzani.

Hadi dakika ya 50 inafika, wachezaji wake – João Cancelo, Kyle Walker, Rodri, Fernandinho na Ilkay Gündogan walikuwa wameugusa mpira mara 288 wakati akina Mahrez, Bernardo Silva, Foden na Silva hawakuwa wameugusa kabisa, wakaishia kuchabangwa 3-1 na kutupwa nje kabisa ya mashindano wajaribu tena msimu ujao.

Mtanange wa nusu fainali utashuhudia RB Leipzig wakicheza na PSG Jumanne hii wakati miamba Bayern Munich watakipiga na Lyon Jumatano hapo hapo jijini Lisbon. Timu kubwa kama Real Madrid na Juventus walitolewa mapema.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Eymael

Eymael Aponda Usajili Yanga

Mwakinyo

Tinampay Amembadilisha Mwakinyo