in , , ,

Pointi 20 zatenganisha timu EPL

*QPR yabaki na pointi mbili mkiani

*Reading, Southampton hali mbaya

*Kadi nyekundu zatawala

*Wachezaji wajifunga

Ilikuwa Jumapili ya kukamiana, lakini mechi mbili zililizochezwa katika Ligi Kuu ya England ziliisha kwa sare ya 1-1.
Queen Park Rangers (QPR) wamezidi kumweka kocha wao mkuu, Mark Hughes ‘Sparky’ kwenye hali mbaya, kwani wanashika mkia katika msimamo.
Wakicheza uwanja wa nyumbani – Loftus Road ulio White City, London, QPR walianza vyema.
Katika dakika ya pili tu, mchezaji wao mpya, Junior Hoilett alipachika bao safi la kuparaza na kuwashitua Everton walio katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Mzunguko huu wa nane umekuwa na balaa la wachezaji kujifunga, kwani golikipa Mbrazili wa QPR aliyesajiliwa msimu huu, Julio Cesar alijifunga.
Ilikuwa dakika ya 33, mpira wa kichwa uliopigwa na
Sylvain Distin wa Everton ulipogonga mti wa goli, kurudi uwanjani kumgonga Cesar na kwenda wavuni kusawazisha mambo.
Licha ya mmiliki wa QPR, Tony Fernandes kudai yupo na kocha wake katika majaribu yanayomsibu na kwamba hali si mbaya kihivyo, uvumilivu unaweza kufikia kikomo karibuni mambo yasipobadilika.
Wamiliki wa timu huwa hawaachi kubadilika kimsimamo, maana wanataka kulinda uwekezaji wao, lakini pia kupata heshima kwa kushinda mechi na ikiwezekana kutwaa vikombe. Mechi ijayo QPR watakaribishwa na Arsenal katika dimba la Emirates.
Kana kwamba ni sikio la kufa lisilosikia dawa, QPR walishindwa kutumia faida ya upungufu wa mchezaji mmoja kwa wapinzani wao, kwani Steven Pienaar alipewa kadi ya nyekundu katika dakika ya 60.
Zimwi la wachezaji kujifunga katika mzunguko huu liliwaandama Newcastle waliokuwa wakiongoza kwa bao moja dhidi ya Sunderland, pale mfungaji mahiri, Demba Ba alipojitwisha kichwa na kutikisa nyavu za timu yake.
Itakumbukwa kwamba Wayne Rooney wa Manchester United alitangulia kujifunga bao Jumamosi kabla ya kurekebisha makosa na kuwafungia United mabao mawili.
Goli la Demba Ba la kujifunga dakika nne tu kabla ya mpira kumalizika, lilifuta kazi nzuri na ngumu waliyofanya Newcastle kwa goli la Yohan Cabaye dakika ya tatu tu ya mchezo.
Mechi hii pia ilikumbwa na mchezaji kutolewa nje, kwani Cheick Tiote alipewa kadi nyekundu mchezo ukiwa karibu nusu, baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Sunderland, Steven Fletcher. Manchester City nao walikumbwa na masahibu ya kadi nyekundu Jumamosi, pale James Milner alipotolewa nje mapema kwa rafu.
Kwa matokeo ya mwisho wa wiki, Chelsea wanaendelea kuongoza wakiwa na pointi 22, wakifuatiwa na Manchester United wenye pointi 18.
Man City ni wa tatu baada ya kujikusanyia pointi 18 pia, wakati Everton wanafuatia kwa pointi 14, wakifungana na Tottenham Hotspur, West Bromwich Albion na West Ham United.
Fulham wanakamata nafasi ya nane kwa pointi zao 13, Arsenal wakifuatia kwa pointi 12 na Swansea wakihitimisha nusu ya kwanza ya juu kimsimamo.
Liverpool wenye pointi tisa wanashika nafasi ya 11, na idadi hiyo ya pointi pia inashikiliwa na Newcastle, huku Stoke City wakiwa nafasi ya 13.
Sunderland ni ya 14 kwa pointi zao saba, Norwich City wanafuatia kwa pointi sita, Wigan wenye pointi tano ni wa 16 na Aston Villa wenye pointi tano wanafuatia.
Southampton wenye pointi nne wanashika nafasi ya nne wanashika nafasi ya 18 wakifuatiwa na Reading wenye pointi tatu, na wote wawili walipanda daraja msimu huu, huku QPR walionusurika kushuka daraja wakishika mkia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Manchester, Chelsea bado wababe

Hakuna suluhu ubaguzi katika soka England..