in , , ,

Pep Guardiola ni mbunifu au mvurugaji vipaji?

Pep Guardiola

PAMBANO la raundi ya 16 mtoano kati ya Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich na Italia, Juventus Turin lilikuwa la kusisimua. Tangu mwanzo wa mchezo kulikuwa na mbinu nyingi za makocha na wachezaji binafsi. Lakini ni Juventus waliofaulu mbinu yao.

Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola kama kawaida yake anapotaka kujilinda alimpanga Medhi Benatia katika nafasi ya beki wa kati akishirikiana na Joshua Kimmich.

Hata hivyo, Kimmich siyo beki wa kati bali kiungo. Kwahiyo Pep Guardiola alimpanga beki mmoja wa kati anayesaidiwa na viungo. Beki wa kulia alikuwa Philip Lahm, na kushoto alicheza David Alaba.

Viungo washambuliaji walikuwa Xabi Alonso, Arturo Vidal, wakati mawinga walikuwa Douglas Costa upande wa kulia na Frank Ribery upande wa kushoto. Safu ya ushambuliaji iliongozwa na Thomas Muller na Robert Lewandowski.

Kipindi cha kwanza JUventus walipata mabao mawili kutokana na makosa ya safu ya ulinzi. Hapakuwa na mawasiliano mazuri kati ya Benatia, Kimmich na Alaba. Hilo lilichangia Benatia kuwa na kiwango kidogo.

Benatia ni beki mzuri anapocheza na beki mwenzake(mfano Jerome Boateng) siyo kiungo kama Kimmich.

Kipindi cha pili Pep Gaurdiola akaja na vituko vyake. Akamtoa Alonso na Benatia kisha nafasi zao zikachukuliwa na Juan Bernat na Kingsley Coman.

Kwa asili Coman ni winga, na Bernat ni beki wa kushoto. Hii ilikuwa na maana aliyekuwa akicheza beki wa kushoto David Alaba alilazimika kucheza beki wa kati (vituko hivi).

Kisha akamwingiza Thiago Alcantara kuchukua nafasi ya Frank Ribery. Mabadiliko ya Thiago yalikwenda eneo sahihi, lakini kitendawili kilikuwa kwa Bernat na Alaba.

Ilimaanisha Pep hakutaka kucheza na beki halisi wa kati badala yake aliwapa majukumu wachezaji nafasi wasizozoea. Joshua Kimmich alibaki kuwa mhimili mkubwa kama beki wa kati.

Kisha Vidal akawa anaipandisha kupanga mashambulizi. Mabao yote mawili ya kusawazisha ya Bayern Munich yametokana na kazi nzuri ya Arturo Vidal. Kisha akapika tena bao la nne lililofungwa na Coman.

Sasa basi, wakati Vidal alikuwa akiingia eneo aliloondolewa Xabi Alonso, maana yake Kimmich alipaswa kucheza namba 4, huku Alaba akicheza namba 5 sambamba na Neuer.

Mwisho kabisa utagundua kuwa Manuel Neuer ndiye sentahafu wa Bayern Munich ingawa wengi wanamwona kama golikipa.

Ukiangalia tofauti ya makipa wa Barcelona na Bayern Munich utagundua kitu kimoja tu; Pep Guardiola amekuwa akipendelea kumtumia golikipa wa Bayern kama mlinzi nambari tano.

Hilo linafanywa kutokana na kipaji kikubwa cha mlinda mlango huyo mzaliwa wa Ujerumani. Kitu hiki kimekuwa kikionyesha tofauti ya Pep Guardiola na makocha wengine. Ndiyo maana sishangai tetesi za kung’olewa Joe Hart pale Manchester City mara baada ya kuwasili Guardiola. Hata hivyo Hart anafaa kunolewa kucheza jukumu la Neuer.

Pep Guardiola
Pep Guardiola

Katika pambano lake na Juventus tuliona maajabu mengine ya Guardiola, alimbadilisha majukumu Douglas Costa kutoka winga wa kulia hadi kucheza nambari 8 kama msaidizi wa Arturo Vidal.

Douglas Costa alikuwa na kazi ya kutengeneza nafasi za kufunga kwa timu, huku akihakikisha Bayern wanamiliki mpira eneo la katikati.

Kulikuwa na mbinu mbili; baada ya kufeli mbinu ya kumiliki mpira kipindi cha kwanza, ndipo Guardiola akabadilisha staili.

Kuingia kwa Coman na Bernat kulimaanisha Bayern itatumia krosi na kushambulia katikati. Kipindi cha kwanza walifeli kupenya ngome ya Juventus katkati. Kipindi cha pili wakaamua kupanua uwanja, Coman anakimbiza kulia na kushoto Bernat alikuwa akipanda zaidi kumsogezea nafasi Douglas Costa pembeni-ndani.

Kuingia kwa Thiago ndipo kulimaliza mbinu za kushambulia kupitia katikati badala ya krosi. Tuliona krosi zilichangia mabao mawili ya vichwa ya Muller na Lowandowski.

Lakini Thiago na Coman wote walifunga kupitia kati kati. Sasa kila ukitazama staili ya ushambuliaji na nafasi walizopangwa wachezaji tunabaki na swali; hivi Guardiola ni mvuragaji wa vipaji au mbunifu? Nadhani huwa anashika ‘remote’ kila anapocheza.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

UWEZO WA BARCA WA KUMALIZIA NAFASI NDICHO KILICHOIUA ARSENAL

Tanzania Sports

SABABU TANO KUWA YANGA WATAWAONDOSHA APR