in , , ,

PAZIA LA EPL KUFUNGWA:

Claudio Ranieri


Chelsea vs Leicester ngoma nzito

*Pata takwimu za bingwa mpya na mtetezi*

*Hiddink na Ranieri wamefuatana klabuni*

Jumapili hii pazia la Ligi Kuu ya England (EPL) linashushwa kwa timu
zote 20, wakiwamo mabingwa na wale watatu wanaoshuka daraja kuingia
dimbani kuikamilisha kazi.

Chelsea waliokuwa mabingwa watetezi watakuwa nyumbani kucheza na
mabingwa wapya, Leicester City. Chelsea walikuwa na nguvu siku
zilizopita, ambapo walishinda mechi sita mfululizo dhidi ya Leicester
kabla ya kuja kufungwa 2-1 kwenye mehi ya awali Desemba msimu huu.

Leicester wanaingia kwenye mechi ya mwisho wakiwa wamepoteza mechi
mbili tu za ugenini kati ya 21 zilizopita. Leicester au Foxes kama
wanavyoitwa wanamaliza ligi wakiwa na pointi nyingi zaidi
walizokusanya ugenini, kwa sasa ni 38.

Chelsea wameshinda mechi tano tu nyumbani kwao msimu huu; nazo zikiwa
ni dhidi ya timu nne zilizo mkiani na Arsenal. Foxes, kati ya mechi
saba walizocheza ugenini siku ya mwisho wa msimu walifanikiwa kushinda
moja tu, lakini hawa ni Mbweha hawa ni wengine, wapo chini ya Claudio
Ranieri.

Katika mechi 11 walizocheza Stamford Bridge, Chelsea wameshinda kuzuia
nyavu zao kutikiswa wakati Leicester wamefungana na Crystal Palace kwa
idadi ya penati walizofunga katika msimu mmoja wa EPL, nazo ni 13. Kwa
Palace ilikuwa msimu wa 2004/5.

Chelsea wamecheza nyumbani kwao mechi nyingi zaidi za EPL siku ya
mwisho wa msimu kuliko timu nyingine yoyote ya ligi hiyo, na wamecheza
mara 15 hapo, wakishinda 11, sare mbili na kupoteza mbili. Ngoma ipo
Jumapili hii.

Claudio Ranieri anaweza kufikisha rekodi ya kushinda mechi 100 katika
EPL Jumapili hii; ambapo historia inaonesha kwamba ameshashinda mechi
99, sare 48 na kupoteza mechi 36, hivyo anaweza kuwa kocha wa 18
kufikia hatua hiyo kubwa.

Ikiwa nahodha wa Leicester, Wes Morgan atacheza dakika zote za mechi
hiyo, basi atakuwa mchezaji wa tatu (asiyekuwa golikipa) tu kucheza
dakika zote za mechi zote za msimu. Wengine ni Gary Pallister msimu
wa 1992/93 naJohn Terry msimu wa 2014/15).

Hii itakuwa mara ya nne katika ligi kuu ya hapa kwa mabingwa kucheza
dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi kwenye mechi ya mwisho ya msimu.
Ilipata kutokea hivyo tena miaka ya 1911/12, 1977/78 na 1988/89.

Mwaka 1912 mabingwa Blackburn Rovers walifungwa na mabingwa watetezi
Manchester United 3-1; msimu wa 1977/78 mabingwa Nottingham Forest
wakaenda suluhu na waliokuwa wakitetea ubingwa – Liverpool.Wakati huo
bingwa alikuwa keshapatikana.
JT
Mei 26, 1989 Arsenal waliingia kuwavaa
Liverpool waliokuwa mabingwa watetezi katika mechi iliyokuwa
imeahirishwa kutokana na matukio ya Hillsborough. Washika Bunduki wa
London walihitaji kupata mabao mawili ili watangazwe mabingwa, na
Michael Thomas akafunga katika dakika ya mwisho kuwapa ushindi huo,
wakatawazwa mabingwa siku ya mwisho.

Leicester wanawazidi Chelsea kwa pointi 31 wakati msimu uliopita
Mbweha hao walimaliza wakiwa nyuma ya Chelsea kwa pointi 46.

Kwenye mechi ya kwanza msimu huu, Leicester walishinda 2-1 kwa mabao
ya Jamie Vardy (34′) na Riyad Mahrez (48′). Loïc Rémy (77′)
aliwafungia Chelsea.
Ratiba ya mwisho ya EPL
Hiyo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Jose Mourinho, kwani kwa kufungwa
huko alifukuzwa kazi, lakini pia ilikuwa mechi ya mwisho ambayo Vardy
na Mahrez wote walifunga mabao. Walipata kuwafunga tena Chelsea msimu
wa 1961/62 na 2000/01.

Kocha wa mpito wa Chelsea, Guus Hiddink na Ranieri walipata kuwa
kwenye timu nyingine tofauti na kukutana dimbani wakati Hiddink akiwa
Chelsea na Ranieri akiwa Juventus ambapo Hiddink alishinda 3-2 msimu
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2008/9, hatua ya 16 bora.

Ranieri amepata kushinda mechi tatu za mwanzo akiwa kocha dhidi ya
timu ya Hiddink. Wote wawili wamepata kuwa makocha Chelsea na Valencia
wa Hispania.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Newcastle, Norwich washuka daraja

Tanzania Sports

PAZIA EPL LAFUNGWA: