in ,

Taifa Stars katika maandalizi ya CHAN

Zikiwa zimebaki siku kadhaa kabla ya mchezo wa kufuzu kucheza fainali za wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN) mwakani nchini Afrika Kusini kati ya Taifa Stars na Uganda Shirikisho la Soka dunia (FIFA), wameipiga stop timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes‘kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Iraq kutokana na hali ya usalama duni nchini Iraq.

Mechi hiyo ilikuwa ichezwe Jumanne ijayo Julai 9 kwenye uwanja wa Erbil City ambao umefungiwa na FiFA kwa muda usiojulikana kutokana na shambulio la bomu ambalo liliwahi kutokea na kuuwa watu wasiokuwa na hatia. Uwanja huo upo kilomita 325 kutoka Kaskazini mwa mji mkuu wa Baghdad.

Uganda ilikuwa na matumaini makubwa na mchezo huo wa kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na raundi ya kwanza ya michuano ya kusaka kufuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ mchezo utakaochezwa Julai 13 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salam na kurudiana Julai 27 Kampala nchini Uganda.

Uganda na Tanzania zitacheza mechi ya kwanza ya kusaka kufuzu kushiriki mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan 2014), Afrika Kusini Julai 13 Dar es Salaam, na kisha kurudiana Julai 27 Kampala.

Taifa Stars chini ya Kocha Kim Poulsen wamekuwa na mafanikio makubwa kwenye uwanja wa nyumbani wakiwafunga mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia, Cameroon na Morocco.

Kupigwa stop kwa mchezo huo kirafiki dhidi ya Iraq itazidisha kitete kwa Uganda ambao imekuwa ikiwapa mazoezi magumu wachezaji wake kwa muda wa saa mbili hadi tatu kabla ya kuanza kuchezea mpira na kujifunza mbinu mbalimbali za kuwadhibiti Taifa Stars.

Akizungumza kutoka jijini Kampala jana, Makamu Rais wa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), Mujib Kasule alidhibitisha Fifa kuipiga stop mchezo huo kufanyika nchini Iraq na badala yake ikiagiza ufanyike nchi nyingine.

“Muda wa kuihamisha mechi yetu kuchezwa nchi nyingine ni mdogo tunajaribu kuzungumza na Rwanda kama itakuwa tayari tucheze nayo kabla hatujaenda Tanzania, tunaitaji sana mechi kwa ajili ya kujenga kikosi kizuri ila kama itashindikana hatutakuwa na jinsi.alisema Kasule

Wakati uganda wakiwa na kihoro cha kufutiwa mechi yake na Iraq na kuhaha kusaka mechi nyingine, Stars imeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Karume chini ya kocha Kim Poulsen na imekuwa ikifanya mazoezi makali kwa muda wa masaa mawili kila siku saa 12 asubuhi tayari kukikabili kikosi hicho cha Uganda.

Hata hivyo kocha wa Stars alisema kuwa mchezo huo ni muhimu sana kwao baada ya kushindwa kwenda kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.

Aliongeza kuwa anaimani na kikosi chake kuwa kitashiriki michuano ya CHAN mwakani kwa kuwa kina vijana wengi ambao wanauwezo mkubwa na kwa sasa wamepata uzoefu kwa kuwa wamekaa wote kwa muda mrefu.

Poulsen alisema kwa sasa hata kuwa na mechi yoyote ya kirafiki kwa kuwa muda ni mdogo anachofanya ila anakuwa anayafanyia kazi mapungufu madogo madogo ilikukiweka kikosi chake katika hali nzuri.

”Naijua Uganda ni timu nzuri na inaupinzani mkubwa lakini tutajitaidi kuakikisha tunashinda mchezo huo nyumbani ili ugenini tusipate shida” alisema.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeteuwa waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya Stars na Uganda.

Waamuzi hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Jean Claude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.

Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Tanzania Yaenda Urusi kwa Riadha Dunia

Athletes Should Perform Better