Simba wamestahili ushindi…

Mechi ya “Nani mtani jembe” iliyozikutanisha Simba vs Yanga imemalizika kwa timu ya simba kupata ushindi wa bao 3-1 mabao ya Simba mawili yakitiwa wavuni na mshambuliaji hatari toka nchini Burundi Amisi Tabwe moja kwa mkwaju wa penati na la tatu likifungwa na Awadhi Juma,wakati lile la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.

Simba waliingia uwanjani wakiwa hawapewi nafasi kubwa kutokana na kikosi chao kutosheheni majina makubwa kama ilivyo kwa watani zao yanga.Simba waliwafumba mashabiki mdomo baada ya Jonas Mkude na mkongwe Henry Joseph,kuwafunika Athumani Idd na Frank Domayo sehemu ya kiungo.

Baada ya simba kukamata kiungo cha yanga,mrwanda Haruna Niyonzima aliyekuwa anacheza winga ya kushoto alilazimika kushuka chini kufuata mipira huku Mrisho Ngassa aliyeanza upande wa winga ya kulia,akikwaa kisiki cha beki Issa Rashidi “Baba Ubaya”.

Beki ya kati ya Yanga inayoongozwa na Kelvin Yongani na Nadir Haroub iliendelea kucheza “Lugha gongana” huku beki ya kushoto David Luhende akizidiwa ujaja na Ramadhani Singano “messi” ambaye leo alikuwa fundi na kila mtu alivutiwa kumtazama.

Golikipa aliyesajiliwa na Simba toka Gor Mahia ya nchini kenya Ivo Mapunda,amefanya kazi nzuri huku beki mkenya Donald Musoti akidhihirisha ubora wake.Musoti ananguvu,akili na uwezo wa hali ya juu wa namna ya kucheza mipira ya juu na chini.

Kituko katika mechi hiyo ya “Nani Mtani Jembe” ni pale Golikipa wa Yanga Juma kasseja alipokataa kupeana mkono na kipa wa simba Ivo Mapunda huku upande wa pili,mashabiki wa simba wakimpigia makofi na kumshangilia Emmanuel Okwi ambaye ni mshambuliaji wao wa zamani na sasa anakipiga kwa watani zao.

Kocha wa simba Loga anaonekana kuwa mtu anayejiamini sana huku akisaidiwa na Suleymani Matola. Pamoja na presha ya mechi kubwa kama hii, amewapa nafasi wachezaji wengi sana na karibu wote wamefanya vizuri.

Posted under:  

Tags:  , , , ,

Comments