in , , ,

Safari ndefu Ligi Kuu Tanzania


*Yanga walitakata, Azam nao, Simba doro
*Sintofahamu bado katika upangaji mechi

KUNA mambo yasiyo ya kawaida yaliyojitokeza kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika Jumamosi ya Mei 18, 2013 kwa Yanga kutia nakshi sherehe za ubingwa wao kwa kuwalaza watani wao Simba 2-0.
Polisi Morogoro  na Toto African ya Mwanza waliungana na African Lyon ya Dar es Salaam kushuka daraja, licha ya timu zote mbili kuwashinda wapinzani wao 2-0 kwenye mechi za mwisho walizocheza nyumbani.
Toto waliwafunga Ruvu Shooting, huku Polisi Moro wakiwafunga Coastal Union ya Tanga na wote kufikisha pointi 25.
Mgambo Shooting waliokuwa na idadi hiyo hiyo ya pointi kabla ya mechi ya mwisho, walisalimika kushuka daraja kwa ushindi wa nyumbani wa 1-0 dhidi ya African Lyon waliokwishashuka daraja kabla ya mechi hiyo wakiwa na pointi 19 walizoingia na kutoka nazo kwenye mechi yao hiyo ya mwisho.
Mgambo Shooting, waliokuwa na pointi 25 kabla ya mechi hiyo ambazo Polisi Moro na Toto wamepigana kwa mafanikio kuzifikia, wameziacha, kufikia pointi 28 na kubaki kucheza ligi kuu msimu ujao.

20130518-190725.jpg

Matokeo mengine ya mechi za mwisho ni washindi wa pili Azam FC kuwashinda JKT Oljoro 1-0 ugenini Arusha, Kagera Sugar ambao wamekuwa wa nne nyuma ya Simba walishinda nyumbani Bukoba 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya na Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro walilala 1-0 kwa Ruvu JKT kwenye uwanja wa Azam wa Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Yapo mambo kadhaa yaliyojitokeza; moja likiwa mchezaji kusaini mkataba na timu nyingine kabla msimu wa ligi haujamalizika na kucheza dhidi ya timu aliyosaini nayo mkataba mpya!
Huyo ni Mrisho Ngassa aliyetangazwa rasmi na uongozi wa Yanga kwamba amesaini mkataba wa miaka miwili kuwachezea wana Jangwani, akitoka Simba alikochezea dhidi ya Yanga kwenye mechi yao ya mwisho.
Suala jingine ni timu zenye malengo mamoja kutofautiana idadi ye mechi mbili. Kuna wakati msimu huu, Mgambo Shooting walikuwa wamecheza mechi 23, wakabakiza mechi tatu, wakiwa na pointi 25 na walikuwa wanahitaji pointi nne toka mechi hizo tatu kuhakikisha hawashuki daraja.
JKT Ruvu, wakati huo walikuwa wamecheza mechi 23, wamebakiza tatu, wakiwa na pointi 23 na walikuwa wanahitaji pointi sita toka mechi hizo tatu wahakikishe hawashuki daraja.
Polisi Morogoro wakati huo walikuwawamecheza mechi 23, wakibakiza mechi tatu, walikuwa na pointi 19, walikuwa wanaweza kufikisha pointi 28 na kutazama walivyosimama wengine. Wangeweza wasishuke daraja endapo wengine wangeteleza.
African Lyon nao kama Polisi Morogoro wakati huo walikuwa wamecheza mechi 23, nao walibakiza mechi tatu, walikuwa na pointi 19,walikuwa wanaweza kufikisha pointi 28 na kutazama walivyosimama wengine. Wangeweza wasishuke daraja kama wengine wangeteleza.
Sasa hali ikiwa hivyo, Toto walikuwa wamecheza mechi 25, wamebakiza moja, walikuwa na pointi 22, walikuwa wanaweza kufika pointi 25 tu wakati huo wakiombea wapinzani wake watatu – Ruvu JKT, Polisi Moro na African Lyon wasifikie pointi hizo au hata wakifika, tofauti ya uwiano wa mabao iwapendelee wao Toto.
Kadhalika, waliomba Mgambo Shooting wasiongeze pointi yoyote toka hizo 25 kwa sababu wao Toto walikuwa na mabao 22 ya kufunga wakati huo na Mgambo Shooting wakiwa na 16. Mgambo wangeweza kuungana na wengine wawili kushuka daraja.

20130502-150313.jpg
Hesabu zote hizo zilikuwa ngumu sana dhidi ya Toto African. Mwishoni, kama ilivyokwishaelezwa, Toto African wameshuka daraja na Polisi Morogoro wakiungana na African Lyon waliokwishaiaga ligi kuu. Kulikoni?
Lipo jingine; hapakuwapo uwiano wa timu kucheza nyumbani na ugenini tangu mzunguko wa kwanza hadi wa pili, hivyo kutokezea timu, kama Yanga, kuecheza sana nyumbani kwenye mzunguko wa pili huku Simba wakicheza zaidi ugenini kwenye mzunguko huo.

Katika mechi 13 za mzunguko huo Yangawamecheza nje ya Dar es Salaam Morogoro dhidi ya Polisi; Arusha kwa JKT Oljoro na Tanga dhidi ya Mgambo Shooting. Huko ugenini katika mzunguko huu walishinda mechi moja dhidi ya JKT Oljoro, wakaenda suluhu na Polisi Morogoro na sare ya 1-1 na Mgambo Shooting. La kujiuliza; ipi athari ya mpango wa mechi kihivyo, nani anafaidi na nani anaumia? Tafakari.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Fergie kocha bora wa mwaka

Kocha mwingine EPL atema mzigo