Oxlade-Chaberlain fiti Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya England imepata ahueni baada ya kubaini kwamba kiungo wao, Alex Oxlade-Chamberlain atakuwa fiti kucheza kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil.

Ox, kama wanavyopenda kufupisha wenzake, aliumia goti kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador Jumatano iliyopita na palikuwa na wasiwasi kwamba mchezaji huyo wa Arsenal angeondolewa kwenye kikosi hicho.

Hata hivyo, Kocha Roy Hodgson amesema kwamba Ox atacheza bila wasiwasi, ikikumbukwa kwamba alikosa mechi kadhaa za Ligi Kuu ya England baada ya kuwa majeruhi. Katika mechi dhidi ya Ecuador matokeo yalikuwa 2-2 na Jumamosi hii walikwenda suluhu na Honduras.

Hii ilikuwa mechi ya mwisho ya maandalizi na sasa wanaelekea Brazil tayari kwa mashindano yatakayoanza rasmi Alhamisi hii. Nahodha Steven Gerrard alieleza kufurahishwa na uwapo wa Ox na kwamba kwenye mechi ya Jumamosi hapakuwa na majeruhi wapya licha ya makabiliano mabaya kutoka kwa wachezaji wa Honduras.

Posted under:  

Tags:  ,

Comments