Liverpool wawafyatua Spurs

*Villa wawafunga Hull
 

Brendan Rodgers amesherehekea mechi yake ya 100 na Liverpool kwa vijana wake kuwafyatua Tottenham Hotspur kwa mabao 3-0.

Uzuri zaidi kwake ni kwamba mechi yenyewe ilifanyika ugenini, White Hart Lane, lakini Spurs hawakuonesha jeuri yoyote, lakini mchezaji wake mpya, Mario Balotelli alipoteza nafasi kadhaa za wazi.

Hii ni mara ya kwanza Spurs wanapoteza mechi chini ya bosi mpya, Mauricio Pochettino aliyehamia London Kaskazini akitoka Southampton. Msimu uliopita wakati kama huu, Liverpool waliwaadhiri Spurs 5-0.

Mabao ya Jumapili hii kwa Liverpool yalifungwa na Raheem Sterling alitefunga kwa kumhadaa kipa Hugo Lloris, la pili likifungwa na Steven Gerrard kwa penati kabla ya Alberto Moreno kupachika la tatu.

Penati ilitolewa kutokana na beki wa kulia wa Spurs, Eric Dier kumchezea vibaya kiungo wa Liverpool, Joe Allen. Sterling aliwahangaisha sana Spurs, akicheza kama mshambuliaji wa kati, kutokana na kasi yake, akienda moja kwa moja golini mara kwa mara.

Katika mechi nyingine, Aston Villa chini ya makocha Paul Lambert na Roy Keane wameendelea kufanya vyema, kwa kuwafunga Hull mabao 2-1. Hawajapoteza mechi tangu kuanza kwa ligi.

Gabriel Agbonlahor alifunga bao la kwanza dakika ya 14 tu ya mchezo, huku Andreas Weimann akifunga katika dakika ya 36 kwa shuti la umbali wa yadi 10. Hull walifuta machozi kwa bao la mchezaji wa zamani wa Everton, Nikica Jelavic lililomgonga kwanza mlinzi wa Villa,  Aly Cissokho kabla ya kujaa wavuni.

Villa walimaliza wakiwa wachezaji 10 tu baada ya Ron Vlaar kuumia na kutolewa nje lakini wakafanikiwa kulinda ushindi wao.

Posted under:  

Tags:  , ,

Comments