Guinea Bissau wavuka AFCON

Hatimaye bahati nasibu imewavusha Guinea Bissau kuingia robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrka (AFCON).

Guinea Bissau walikuwa wamefungana na Mali kwa pointi, mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo kulazimisha bahati nasibu kufanyika kupata wa kuvuka.
Hata hivyo, mataifa yote mawili yalikuwa yanapinga mtindo wa kutumia bahati nasibu, badala yake walitaka warudiane ili mshindi apatikane uwanjani.

Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), hata hivyo, lilishikilia uamuzi wake wa kuendelea na droo hiyo, lakini linafikiria kwa siku zijazo kuwa na mechi ya mtoano ikiwa timu zinafungana, jambo ambalo halitokei mara nyingi.

Guinea Bissau na Mali wote walitoka sare ya 1-1 katika mechi tatu tofauti kwenye michuano hiyo na kuwaweka sawa, kitu ambacho hakijatokea kwa timu yoyote tangu 1988 Algeria walipokwenda sare na Ivory Coast, kisha bahati nasibu kuwavusha Algeria.

Katika kundi hilo la D, Ivory Coast walimaliza wakiwa wa kwanza kwa pointi tano, Guinea na Mali pointi tatu huku Cameroon wakimaliza wakiwa na pointi mbili tu, yakiwa mashindano waliyofanya vibaya zaidi.

Mwakilishi mmoja mmoja kutoka Guinea na Mali walishiriki kwenye droo hiyo ambapo watu walikuwa wakichagua vitufe kutoka kwenye sahani. Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mali,
Boubacar Diarra alikuwa wa kwanza, akachagua kitufe kilichowaweka wa tatu, akaanza kulia.

Mkurugenzi wa Fedha wa Chama cha Soka cha Guinea Bissau, Amara Dabo alikwenda kwenye sahani na kuchukua kitufe kilichowahakikishia kuwa katika nafasi ya pili. Wanapochukua vitufe hivyo huwa hawatazami, bali hukisia tu.

Mchezaji wa zamani wa Mali, Tottenham Hotspur na West Ham, Frederic Kanoute (37) alieleza kusikitishwa kwake kwa kutumia bahati nasibu kuchagua mtu wa kuvuka, badala ya kupambana dimbani, akisema huo si mchezo, lakini akawasifu ndugu zao wa Guinea Bissau.

Posted under:  

Tags:  

Comments