in , , ,

Dunga aisuka upya Brazil

 

*Afyeka nyota 13 wa zamani

Kocha mpya wa Timu ya Soka ya Brazil, Dunga, ameanza kazi kwa kutema wachezaji kadhaa na kuchagua wengine kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Colombia na Ecuador, akiweka msingi mpya wa kazi yake.

Dunga aliyechukua nafasi iliyoachwa na kocha aliyeachia ngazi, Luiz Felipe Scolari, amemwacha kipa wa siku nyingi, Julio Cesar, lakini pia beki wa kulia wa Barcelona, Dani Alves; Marcelo wa Reakl Madrid na Paulinho wa Tottenham Hotspur.

Makipa aliowaita ni Jefferson wa Botafogo na Rafael wa Napoli. Mabeki na majina ya timu zao kwenye mabano ni Maicon (AS Roma), Filipe Luis (Chelsea), Alex Sandro (Porto), Danilo (Porto), David Luiz (Paris Saint-Germain), Marquinhos (Paris Saint-Germain), Gil (Corinthians) na Miranda wa Atletico Madrid.

Viungo ambao Dunga ataanza nao ni  Fernandinho (Manchester City), Luiz Gustavo (VfL Wolfsburg), Elias (Corinthians), Ramires (Chelsea), Everton Ribeiro (Cruzeiro), Ricardo Goulart (Cruzeiro), Oscar (Chelsea), Willian (Chelsea) na Philippe Coutinho  wa Liverpool.

Kwenye safu ya ushambuliaji watakuwapo Hulk wa Zenit St Petersburg, Neymar wa Barcelona ambaye yupo fiti baada ya kuteguliwa vifundo vya mgongo kwenye mechi ya fainali za Kombe la Dunia na mshambuliaji mwingine ni Diego Tardelli kutoka Atletico Mineiro.

Coutinho ameitwa tena kwenye kikosi cha Brazil baada ya kuonesha mpira maridadi akiwa na Liverpool lakini nahodha Thiago Silva atakosa safari hii kutokana na kuwa majeruhi. Brazil walishika nafasi ya nne kwenye fainali za Kombe la Dunia, baada ya kuchapwa mabao saba na waliokuja kuwa mabingwa, Ujerumani.

Wakiwa wenyeji, raia wa Brazil ambao ni vichaa wa soka, waliona kwamba timu yao iliwaangusha na kocha akaamua mwenyewe kuachia ngazi, japokuwa kulikuwa na kila dalili kwamba angeondoshwa. Hii ni mara ya pili kwa Dunga kushika nafasi hiyo, ambapo amepata kuichezea timu hiyo ya taifa na kutwaa mataji nayo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal, Besiktas ngoma mbichi

Barcelona waangukia pua