Michezo ya Bandari Kutimua Vumbi Jijini Mwanza

Mashindano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari maarufu kama ‘Interports Games’ yanatarajiwa kutimua vumbi jijini Mwanza kuanzia Oktoba 15 hadi 19, mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba.
Meneja Mawasiliano, Bw. Franklin Mziray amesema michuano hii inatarajiwa kuwa ya vuta ni kuvute ambapo Bandari zote zilizopo chini ya usimamizi wa TPA zitawania vikombe na zawadi mbalimbali za ushindi.
“Michuano hii ina historia ya kuwa na ushindani mkubwa baina ya bandari, tunatarajia kuwa pamoja na kuleta ari ya kupenda michezo na kutujenga afya zetu pia itakuwa ni kivutio cha aina yake kwa wakazi wa jiji la Mwanza katika wiki yote ya mashindano haya,” anafafanua Mziray.
Mziray amewakaribisha wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake pamoja na wadau wote wa michezo, kujumuika na wanabandari katika kupata burudani ya aina yake. Mashindano haya hayatakuwa na kiingilio na watu wote wanakaribishwa.
Michezo itakayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa soka, riadha, mpira wa kikapu, mpira wa pete, kuvuta kamba na bao. Bandari zitakazoshiriki katika michezo hii ni pamoja na Bandari Dar, Bandari Mtwara, Bandari Tanga, Bandari Mwanza na Makao Makuu ya TPA.

Posted under:  

Tags:  

Comments