in , , ,

NILICHOKIONA KWENYE BAADHI YA MECHI ZA EPL.


LIVERPOOL vs SWANSEA CITY.

Katika hii mechi, Swansea City walionekana kama timu ambayo inataka
kubaki kwenye ligi wakati Liverpool ilionekana kama timu isiyo kuwa na
shida na ubingwa.

Ndiyo maana hata kipindi cha kwanza Liverpool hawakufanikiwa kuwa na
shot on target hata moja.

Kitu ambacho kilileta ugumu wa mechi hii ni kwamba, walipokuwa
wanapata mipira walijitahidi sana kubaki nao bila kupoteza ovyo, hata
wakati ambao walikuwa hawana mpira walijitahidi sana kuutafuta na hii
iliwanyima uhuru Liverpool.

Kitu kikubwa ambacho Liverpool wanatakiwa wakiangalie sana kipindi
hiki ni kwenye eneo lao la mabeki.

Mabeki wao wanakosa vitu vifuatavyo : Cha kwanza ni marking mbaya,
pili siyo wazuri wa kucheza mipira ya juu na ya krosi.

Kwa kiasi kikubwa Liverpool walimkosa Mane, hasa hasa pale timu
ilipokuwa inahitaji mtu wa kulazimisha mashambulizi kwa kasi.
Countinho bado hajapata Match fitness.

STOKE CITY vs MANCHESTER UNITED.

Charlie Adam na Whilan, ni kati ya viungo ambao Kwenye mechi hii
waliongeza ugumu, Kwa sababu kumwanzisha Fellain katika eneo la kiungo
kulikuwa na maana ya kuwafanya viungo wa Stoke City wasiweze kutembea,
lakini haikuwa hivo kama alivyotegemea Mourinho.

Goli la kujifunga la dakika za Mwanzo liliwapa nguvu sana Stoke City
kwenye eneo la kujilinda. Walikuwa na nidhamu kubwa sana eneo hili,
kitu ambacho kiliwafanya Manchester United kuhangaika sana.

Sitaki kuzungumzia record aliyoiweka Rooney ya kuwa mfungaji bora wa
wakati wote wa klabu. Kitu kikubwa ninachotaka kukuzungumzia ni jinsi
goli lilivyofungwa.

Kuna vitu vingi vimekuwa haviangaliwi sana, ni nidhamu ya ufundi.Moja
ya nidhamu ya ufundi katika mpira ni jinsi unavyotumia kila nafasi
kama za adhabu ndogo, kona ili kupata magoli. Kwa utulivu aliokuwa
nao Rooney kabla ya kupiga ile adhabu ndogo mpaka akafunga hii ndiyo
tunaita nidhamu ya ufundi.

MANCHESTER CITY na SPURS.

Hutakiwi kuwadharau Spurs, hutakiwi kuwachukulia katika udogo hawa
watu. Kwani tayari wameshakomaa na wako katika daraja alilopo Chelsea,
tena usishawishike kuwaweka daraja alilopo Manchester City na ndugu
yake Manchester United.

Kiwango cha Hugo Lloris kilikuwa kizuri kipindi cha kwanza, makosa
aliyoyafanya kipindi cha pili yaliigharimu timu, lakini kitu kizuri
timu ilitulia, ikarudi nyuma ya magoli mawili.

Kitu kikubwa ambacho kiliwasumbua sana Spurs kwenye mechi hii ni pengo
la Vertonghen. Pochettino alijaribu kutumia mfumo wa mabeki watatu ili
kuziba pengo hili, lakini hakufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kumwanzisha Kelvin De Bryune katikati ya uwanja kiliwafanya Dembele na
Wanyama kuwa na kazi moja tu kuwazuia Kelvin na Silva, kitu
kilichosababisha Erricksen na Delle Ali kutopata mipira mingi sana
kipindi cha Kwanza.

Kilichokuja kuwasaidia Spurs ni pale walipoamua kutumia mabeki wanne,
kitu kilicholeta uhai eneo la kujilinda, hivyo wakaamua kutumia
mipira mirefu na krosi wakijua kabisaa mabeki wa Man City hawana uwezo
mkubwa wa kuzuia mipira ya juu. Na ikawa faida kwao kupata magoli ya
kusawazisha.


Arsenal na Burnely.

Burnely aliingia kwenye mchezo huu kwa ajili ya kuzuia na kushambulia
kwa kushtukiza kwa kutumia mipira mirefu.
Arsenal waliliona hilo walichoamua kufanya ni wao kuhakikisha wanakuwa
na mipira wakati mwingi ili wawanyime Burnely nafasi ya kupata mipira
na kucheza mipira mirefu.

Arsenal walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukaa na mpira, tatizo kubwa
kwao lilikuwa ni jinsi ya kupita kwenye ukuta wa Burnely ambao kwa
kias kikubwa ulikuwa mgumu.

Option kubwa ambayo walitakiwa kuitumia ni wao kupiga mipira ya krosi
lakini wao wakawa wanataka kupitia katikati ambapo palikuwa na ugumu.

Xhaka anatakiwa awe na nidhamu kubwa kama anataka kuwa mchezaji mwenye
kiwango cha juu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

AFCON: HAISHANGAZI UGANDA KUONDOLEWA MAPEMA

Tanzania Sports

YA MONTELLA NA ALLEGRI YANA HUZUNISHA UKIYAKUMBUKA YA CAPELLO NA ANCELOTTI