in , , ,

NILICHOKIONA KWENYE BAADHI YA MECHI WEEK-END HII

Inawezekana wazo la kuwaanzisha Iwobi, Welbeck, Oxlaide Chamberlain
pamoja na Giroud lilikuwa wazo zuri lakini halikufanikiwa kwa kiasi
kikubwa.

Kwa msimu huu moja ya matatizo yaliyokuwa yanaikumba Liverpool ni
uwezo wa safu ya ulinzi ya Liverpool kutokuwa madhubutu na mipira ya
juu inayotokana na mipira ya krosi

Kuwaanzisha Welbeck, Oxlaidé na Iwobi kulikuwa na maana kuwa Arsenal
ingenufaika zaidi na kasi pamoja na mipira ya krosi ambayo Giroud
angeweza kuitumia kwa sababu ni mzuri kwenye mipira hiyo lakini wazo
hilo halikufanikiwa kwa sababu zifuatazo.

Moja: Kuwaanzisha Xhaka na Francis kwa pamoja inakuwa na hasara kubwa
sana Kwa Arsenal kwa upande wa kushambulia. Kwanini nasema hivo ?
Xhaka na Francis wote Kwa pamoja kiuhalisia ni viungo wenye sifa
nyingi za kukaba, hivo Kuwaanzisha wote kwa pamoja unakuwa huna
uhakika mkubwa wa timu kupata mipira mingi kwenye nusu ya eneo la
mpinzani. Ndicho kitu kilichotokea jana, timu haikupata mipira mingi
kwenye nusu ya eneo la Liverpool na hii ikawafanya kina Welbeck na
Oxlaidé kutopata mipira mingi kwa ajili ya kupiga krosi kwa Giroud.

Iwobi hana sifa nyingi nzuri za kuwa namba kumi bora maana hakuweza
kumchezesha kwa kiasi kikubwa Giroud na hii ilitokana na mambo mawili,
moja ni kukosana kiungo bora mchezeshaji wa kati, pili Iwobi kutokuwa
na ubunifu mkubwa wa kupiga pasi za mwisho

Pili: Kwa kiasi kikubwa Emre Can alijitahidi kuwafanya viungo wa kati
wa Arsenal kutokuwa huru kuwa na mipira, hali iliyoleta uhaba wa
mipira kwenye eneo la mbele la Arsenal hasahasa kipindi cha kwanza.

Nacho Monreal kadri siku zinavyozidi kwenda anazidi kushuka kiwango
chake na hii ni kwa sababu mbili, moja ametumika sana kwenye misimu ya
hivi karibuni. Mbili Umri wake umeenda sana.

Pamoja na kwamba Liverpool walishinda ila walimkosa mtu wa kuiamrisha
timu kwa pasi zake. Henderson ni mtu muhimu katika hili, mara nyingi
uwepo wake huifanya Liverpool icheze kulingana na amri yake, lakini
Emre Can alikuwa mzuri zaidi kwenye kuzuia na siyo kwa kuiamrisha
timu.

Kitu pekee ambacho Arsenal wamekuwa wakiwa wanahangaika nacho hasahasa
kwenye safu yao ya ulinzi ni kwamba timu imekuwa ikishindwa kujipanga
vizuri pindi inaposhambuliwa kwa kasi pili Arsenal siyo wazuri wa
kukaba kwenye mashambulizi ya kushtukiza.


MANCHESTER UNITED vs AFC BOURNAMOUTH.

Haikuwa siku nzuri kwa Zlatan kwa sababu alikosa nafasi nyingi sana za
wazi pamoja na Penalty.

Manchester United walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwafanya AFC
Bournamouth wasiweze kumiliki mpira kama ilivyosifa yao kubwa na hii
ni kutokana na uwepo wa Carrick.

Carrick alitoa pumzi ya eneo la katikati mwa Afc Bournamouth ambalo ni
uti wa mgongo wao katika kumiliki mpira. Alipoza vizuri mashambulizi
na kuanzisha vizuri mashambulizi ya Manchester United.

Inawezekana Jones na Rojo walifanikiwa kutengeneza ukuta imara kipindi
ambacho Baily na Smalling walipokuwa hawapo. Lakini kuna kitu Kimoja
ambacho kinatakiwa kichukuliwe kwa tahadhari kubwa sana kwenye hii
combination ya Rojo na Jones, wote ni wazito.

Siku wakikutana na washambuliaji wenye wa kati wenye kasi itakuwa hatari sana kwao, King
na Afobe walijaribu lakini kukosa umakini na kuwa na papara
kuliwafanya wasifanikiwe kulingana.

Ubora wa Mata huonekana zaidi anapotokea katikati ya uwanja au
anapocheza nyuma ya mshambuliaji. Kipindi cha kwanza Mata hakuonekana
bora alipokuwa anatokea pembeni lakini mara baada ya kuhamishwa na
kupelekwa katikati tulianza kumshuhudia Mata.


LEICESTER CITY vs HULL CITY.

kitu pekee kilichokuwa kinakosekana kwenye leicester ya Ranieri ni
uwezo wao kupigana.Kitu hiki ni moja ya sababu iliyoibeba Leicester
City kwenye mechi mbili zilizopita. Wachezaji wanaonekana wakiwa
wanacheza Kwa kujituma zaidi.

Goli la mapema là Hull City halikuwatoa mchezoni.

Pia kuna baadhi ya Wachezaji ambao viwango vyao vimefufuka mfano mzuri Mahrez.

Ubora wa Mahrez Kwa sasa unatokana na sababu mbili.

Ya kwanza ni ubora wa safu ya kiungo iliyochini ya Ndindi na
DrinkWater. Ndindi alikuwa mzuri katika kutimiza majukumu yake ya
kuilinda safu ya ulinzi ya Leiceter Çity na kumwacha DrinkWater awe
huru kugawa mipira kwa kina Mahrez, Albrighton, Vardy.

Na kupitia huu wa mipira ndipo kitu cha pili cha kuongezeka Ubora wa kina
Mahrez kinapokuja. Na kitu chenyewe ni wao kujituma zaidi na
kuongezeka Kwa kasi yao na ubunifu wao.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Mechi hizi kuipa Simba ubingwa msimu huu

Tanzania Sports

ARSENE WENGER AAMBIWA: