in , , ,

Ni ‘vita’ Uefa na Fifa

Ni ‘vita’ Uefa na Fifa

Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) linasisitiza juu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) ya msimu wa majira ya joto, hatua inayoweza kuziathiri klabu za Arsenal, Chelsea na Tottenham Hotspur.

Chombo hicho chenye dhamana ya soka barani Ulaya kinaonekana kuzidi kuvimbiana na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) juu ya kalenda ya mashindano ya soka ya kimataifa kwa kuridhia kutanua International Champions Cup.

Inaelezwa kwamba tayari baadhi ya klabu kubwa za Ligi Kuu ya England (EPL) zimeunga mkono mpango huo na zinataka kushirikishwa kwa karibu zaidi.

Mashindano hayo ambayo yatakuwa yanafanyika kabla ya kuanza msimu mpya wa soka kwa ligi nyingi hasa za Ulaya ni kama kupambana na kutaka kuchukuliwa uzuri zaidi kuliko Kombe la Dunia la Klabu – mashindano yanayosogezwa mbele ili kufanyika Juni na Julai 2021 kwa kuanzia huko Shanghai, China.

Mawazo ya michuano mipya ya mfumo wa UCL yanatokana na mawazo yua wadhamini wa Kimarekani – Relevent Sports. Kampuni hiyo imekuwa ikiendesha International Champions Cup tangu 2013. Arsenal, Manchester United na Spurs walishiriki kwenye International Champions Cup mwaka jana.

Haya yanakuja wakati Fifa wakiwa wamepanga kuja na mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu kufikia hadi timu 24 na kuchukua muda zaidi. Mpango wa Uefa ni tishio kwa Fifa, hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji mahiri wengi zaidi na hata klabu maarufu zaidi zipo Ulaya.

Hili linakuja wakati tayari Afrika walionekana kulalamikia mpango huo wa Fifa, kwa sababu nao walikuwa wakijipanga kupangua kalenda ya mashindano yao ili kukidhi kiu ya baadhi ya wadau wa ndani.

Uefa wapo tayari kushirikiana na wadau kwa ajili ya mashindano ya upande wao, ikiwa ni pamoja na kuwapa chapa na logo zao, japokuwa si lazima washiriki moja kwa moja kuyaendesha kimamlaka.

Ushiriki humo utazingatiwa kwa vigezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na nafasi ya timu kwenye msimamo wa ligi za nyumbani (nchi) badala ya mfumo wa sasa wa kualikwa tu kutokana na mvuto wa klabu na wachezaji wake. Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuongeza hadhi ya mashindano husika.

Tayari makubaliano yamefanyika kwamba mashindano hayo yafanyika kila mwaka, na mkataba wa miaka minane umetiwa saini, ambapo kwa kuanzia mashindano yatafanyioka Marekani na kwa miaka ijayo yatakuwa barani Asia.

Kampuni ya Relevant Sports utatoa fungu la fedha kwa mpango wa awali wa kuendesha mashindano hayo, kwa matazamio kwamba kadiri siku zinavyokwenda dili nono zaidi zitapatikana kwa wadhamini kuingia na kuanza kutengeneza faida.

Uwezekano wa kujitanua ni kwamba timu za Amerika Kusini zinaweza kuhusishwa na tayari Uefa wamejisogeza kwa kutia saini mpango wa ushirikiano zaidi na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (Conmebol).

Kadhalika tayari kamati ya mikakati kwa mashindano hayo imeshatengenezwa, ikihusisha wawakilishi wa klabu kubwa kwa ajili ya kufanyia kazi baadhi ya mambo na kuja na mipango mizuri zaidi, kama vile idadi ya timu na nchi za kushirikishwa.

Mashindano ya Fifa, kwa upande mwingine, ambayo ni kwa klabu, yatakuwa yakifanyika kila baada ya miaka minne, lakini kwa haya ya mwakani tayari kuna hisia za kutokea mkanganyiko na mvutano miongoni mwa maofisa wa mashirikisho husika.

Hayo ya Fifa yatahusisha timu 24, zikiwamo 12 kutoka Ulaya, mbili kutoka England na kwa maana hiyo klabu sasa zitapenda kujielekeza zaidi kwenye ile ya Uefa. Tayari Fifa wana matatkwa sababu wanashindwa kupata pauni milioni 650 zinazotakiwa kwa ajili ya kugharamia mashindano, ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi kwa washindi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Chama ndiye Mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba

Tanzania Sports

Yanga inawahitaji MHILU na MAKAMBO kuifunga SIMBA