in ,

NI UWEZO WA ZIDANE AU BAHATI ?

Taarifa za kutimuliwa kwa kocha Rafael Benitez zilionekana za kiuonevu sana.

Asilimia kubwa ya watu waliona Perez alifanya kitu kitu kisicho na
uungwana kwa kumfukuza kocha ambaye alikuwa ameiongoza timu kushinda
mechi 17 kwenye mechi 25 huku akifungwa mechi tatu tu.

Ulikuwa ukichaa wa Perez kumfukuza Benitez, watu wengi waliona hivo.

Wakabeza ukichaa wake, wakalaini ukatili wake na wakakemea uonevu wake.

Maisha kwa Benitez yaliendelea nafasi ya kulizisha nafsi ya kila mtu
kwake hakuwa nayo.

Kwake yeye kuoneka kichaa mbele ya macho ya wengi ilikuwa sawa tu.

Na kwa kuwaumiza wengi ukichaa wake aliuzidisha kwa kumchagua Zidane
kama kocha wa Real Madrid.

Mtu ambaye hakuwa na historia nzuri ya kufundisha mpira katika kiwango kikubwa.

Kuwa kocha msaidizi kwa mwaka mmoja chini ya Carlo Ancelotti
hakukutosha yeye kuaminiwa na wengi
Wengi tulimbeza, tena tulipofikiria kuwa Perez ni mwanadamu ambaye
hakuumbiwa kuvumilia vitu vibaya ndipo hapo tulimpa nafasi ndogo ya
kuishi Real Madrid.

Sekunde zilianza kuruhusu muda usogee ili kutupa jibu sahihi .

Wengi tuliamini Zidane hatokuwa na uwezo mkubwa wa kupata mafanikio
makubwa kama aliyowahi kuyapata wakati akiwa mchezaji.

Miezi 19 imepita , kabati lake ƙlina vikombe sana.

Mafanikio ambayo ni makubwa sana kwake.

Mafaniko ambayo kayapata kwa haraka bila watu kutegemea.

Hakuna mtu aliyetegemea kama angefanya haya ambayo tumeyashuhudia.

Kila mtu alitegemea uhai mfupi wa Zidane pale Madrid.

Ndiyo maana hata mafaniko yake yamekuwa magumu sana kukubarika kwa
uharaka kwa watu, kwa sababu watu wengi waliamini hatoweza kufanya
chochote kikubwa.

Hata baada ya mafanikio yake wengi wetu tumekuwa tukiamini kuwa ana
bahati kubwa kwa sababu amekutana na wachezaji bora kwenye kikosi cha
Real Madrid.

Wachezaji ambao Carlo Ancelotti aliwatumia na kupata makombe 4 ndani
ya miaka 2, wakati Zidane akiwatumia wachezaji hao hao na kupata
makombe 7 ndani ya miezi 19.

Ni Zidane huyu ambaye kwa kiasi kikubwa ameondoa ile hofu ya Real
Madrid bila Ronaldo haiendi.

Timu inacheza kitimu bila kutegemea uwezo wa mtu kwa kiasi kikubwa.

Mchezaji mzuri anapokosekana hakuna kinachobadirika kwenye timu.

Ingekuwa ngumu kuniaminisha kuwa RealMadrid inaweza ikaenda bila
Casemiro, lakini Zidane kanipinga kupitia Kovacic.

Zidane amefanikiwa kutengeneza na kufundisha timu ya wachezaji wote na
siyo kufundisha na kutengeneza kikosi cha kwanza.

Kila mchezaji anayepata nafasi anaonekana ana njaa ya mafanikio.

Zidane kacheza mpira katika kiwango cha juu, kauishi mpira kwa kiasi kikubwa.

Kila mchezaji anatamani katika kiwango alichocheza yeye.

Anachofanya ni wao kuwapa nafasi ya kucheza huru wanavyotaka.

Kambadirisha Isco kutoka kuwa kiungo wa kati wa ushambulizi mpaka kuwa
mchezaji anayetokea pembeni na kuwa huru zaidi kuingia katikati ya
uwanja mpaka eneo la karibu na washambuliaji.

Kawaacha wachezaji wacheze mpira kwa uhuru tena kwa kuwakumbusha
kutumia miguu yote miwili ipasavyo.

Modric amekuwa huru katikati mwa uwanja, Kroos ubunifu wake umeongezeka zaidi.

Zidane amekuwa mtu anayemwamini kila mchezaji katika kikosi chake.

Kwake wachezaji wake 24 wote wana umuhimu na ana waamini.

Kawaamini, kawalisha njaa na wao wamekuwa waogo kumwangusha kila
wanapopata nafasi, ndiyo maana ni virahisi sana kwa Asensio au lucas
Varqez kuonekana bora kwa sababu wameaminishwa wao ni bora.

Kuongoza na kuwasimamia wachezaji wote wakakutii na kuwafanya wacheze
vizuri ni jambo gumu sana lakini Zidane ameweza na ametengeneza jeshi
kubwa linaloogopeka kwa sasa.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

EPL 2017/18 Pazia kushushwa Ijumaa

Tanzania Sports

TUMSOME , TUMWANDIKE NA KUMWELEWA SIMBU