in

Ni lini Aishi Manula tutamuuza nje ?

Aishi Manula

Baada ya kukaa miaka 39 bila kufuzu michuano ya Afcon , mwaka 2019 Tanzania tulifanikiwa kufuzu michuano hiyo iliyofanyika nchini Misri. Hili lilikuwa tukio kubwa sana kwenye mpira wetu, kabla ya hapo mara ya mwisho tulifuzu mwaka 1980.

Pamoja na sisi kuishia kwenye hatua ya makundi kwenye michuano hiyo ya Afcon lakini kuna kitu kimoja ambacho binafsi sitokisahau kwenye michuano hiyo, kitu chenyewe ni uwezo wa Aishi Manula.

Aishi Manula alifanikiwa kutoa michomo mingi kwenye michuano hiyo ya Afcon katika hatua ya makundi. Pamoja na kwamba tulitoka kwenye hatua ya makundi lakini Aishi Manula alikuwa kipa ambaye alitoa michomo mingi kwenye hatua hiyo ya makundi.

Kabla ya sisi Tanzania kufuzu kwenye michuano ya Afcon mwaka 2019, Simba SC walifanikiwa kufika katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika katika msimu wa mwaka 2018/2019.

Katika msimu huo Simba walipokea vipigo vitatu vikubwa. Kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huo wa mwaka 2018/2019, Simba SC alifungwa goli 5-0 dhidi ya As Vita.

Pia timu ya Al Ahly ya nchini Misiri iliwafunga Simba SC goli 5-0 nchini Misri. Simba SC kwenye mechi ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika walikutana na TP Mazembe ambapo walifungwa goli 4-1.

Kwenye vipigo vyote hivo vitatu alivyopokea Simba SC kuna shujaa mmoja ambaye alibakia licha ya kufungwa goli 5-0 , Aishi Manula aliokoa michomo mingi ambayo aliisaidia Simba SC kupunguza idadi ya magoli.

Aishi Manula alionesha uwezo mkubwa wa kutoa michomo mingi licha ya kwamba Simba SC kufungwa magoli mengi. Mwaka huu timu yetu ya taifa ilishiriki michuano ya CHAN.

Michuano ambayo tulitoka kwenye hatua ya makundi. Kama ambavyo ilivyokuwa kwenye michuano ya Afcon pia tulitoka kwenye michuano ya CHAN kwenye hatua ya makundi.

Pamoja na kutoka kwenye hatua ya makundi Aishi Manula alitoa michomo mingi kwenye hatua makundi. Aishi Manula amekuwa mkomavu ni mchezaji ambaye anaweza kuiweka timu yake ndani ya mchezo.

Jana Simba Sc walikuwa wanacheza katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya As Vita. Moja ya wachezaji ambao walikuwa waliiweka Simba SC ndani ya mchezo ni Aishi Manula.

Aishi Manula alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuondoa michomo ambayo iliiweka Simba SC ndani ya mchezo. Huu ndiyo wakati mzuri wa Aishi Manula kumuuza nje ya nchi kwa sasa.

Tushapeleka wachezaji wengi nje ya nchi. Wachezaji ambao wanacheza eneo la ndani ya uwanja, lakini hatujabahatika kupeleka kipa kwenye ligi za nje. Aishi Manula kwa ukomavu aliofikia ni sahihi kwake kucheza ligi ya nje.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Scott McTominay

Manchester United wanaugua ugonjwa wa Liverpool?

Tanzania Sports

Mikel Arteta anataka nini kwa mshambuliaji wake?