in , ,

NI KWANINI ARSENE WENGER ALIMUONYA ALEXIS SANCHEZ KUHUSU FEDHA?

Alexis Sánchez

Kipindi kama hiki cha Krismasi miaka miwili iliyopita niliandika kuhusu namna fedha nyingi zinavyozagaa dunia ya ligi mbalimbali za Ulaya. Desemba 2014 tuliona wachezaji matajiri wenye mishahara inayoanzia paundi za Uingereza laki mbili elfu kwa juma, kuendelea. Hizi ni zaidi ya dola milioni moja na nusu kwa mwezi. Wachezaji niliowaangalia walikuwa Wayne Rooney (£300,000), Lionel Messi (£292,000), Cristiano Ronaldo (£288,000), Robin Van Persie (250,000), Yaya Toure (£230,000), Luis Suarez (£220,000), Sergio Aguero (£220,00) na David Silva (£200,000). Haya ni malipo yanayochanganya mchezaji kutangaza biashara za makampuni mbalimbali kwa mfano Adidas. Ni pia baada ya kukatwa kodi.

Kutokana na mishahara hii wachezaji wengi sasa hivi huongozwa zaidi na tamaa ya fedha kuliko klabu, soka au hata furaha ya kimaisha.

Hiyo ndiyo sababu iliyomfanya kocha wa Arsenal, bwana Arsene Wenger, kumuonya mshambuliaji Alexis Sanchez wa Chile mwanzoni mwa juma hili. Sanchez anayewika kipindi hiki Arsenal amebakisha mwaka mmoja na nusu tu kusaini mkataba mpya. Mshahara wake ni mdogo ukilinganisha na hao niliowataja juu. Anapokea paundi 130,00, ambazo ukimwacha Merzut Ozil (140,000) ni nyingi zaidi ya wachezaji wengine wa Arsenal. Karibuni Ozil ameahidiwa kuongezewa mshahara wa juma kuwa paundi 160,000.

Wenger alichomshauri Sanchez ni kuacha kuangalia fedha anapotaka kuongeza urefu wa mkataba wake na Arsenal.
“Leo hii, “ Wenger alishauri, “popote pale mwanasoka atakapocheza atapata fedha nzuri. Hivyo kwa mtazamo wangu ni bora mchezaji akiangalia zaidi mahitaji na maslahi yake. Aaangalie namna klabu inavyothamini wachezaji, matakwa na malengo yake. Kwangu hilo ni muhimu kwa vile popote pale kuna pesa siku hizi.”

Wenger ana uzoefu wa muda mrefu na ligi za Ulaya. Anafahamu namna wachezaji wanavyojiharibia. Chukua mfano wa wachezaji wake waliokimbia shauri ya uroho wa fedha. Samir Nasr aliuzwa klabu ya Man City. Licha ya mshahara mkubwa zaidi (120,000) hakuja juu kiasi kilichotakiwa kama wenzake Sergio Aguero(220,000), Raheem Sterling (180,000) , Yaya Toure (220,000) na Kevin De Bryune (150,000). Hatimaye amekodishwa (si kuuzwa) klabu ya Sevilla toka Spain.Mwingine ni Cerc Fabregas ambaye baada ya kung’aara kwa muda Chelsea sasa hivi inaelekea hatakiwi. Anataka kurudi tena Arsenal. Au Ruben Van Persie aliyenunuliwa na Man United akakaa miaka mitatu sasa hasikiki aliko, ingawa anacheza Uturuki. Angekaa bado Arsenal si angekuja kusifika kama Thiery Henry?

Klabu mbili zinazoongoza dimba la England ni Chelsea na Man City. Ingawa Liverpool inasogelea karibu karibu, Chelsea na Man City zimepigana miaka kadhaa sasa kuwa klabu zinazotisha. Kinyume na Man United, LIverpool au Arsenal- klabu hizi hazikuwa zinatisha au tuseme hazikujengwa na makocha kama Arsenal na Man United.

Zilijengwa na utajiri wa Mrusi Roman Abramovich na Sheikh Mansour. Matajiri hawa wageni Uingereza wamegeuza namna mpira ulivyo. Sasa hivi mashabiki wa soka wamesahau kabisa kuwa klabu hizi mbili zilijengwa kwa fedha si kwa mpira. Lakini hatimaye klabu hizi zinawika. Lakini haina maana zinajenga wachezaji. Hata zikishinda vikombe, je ina maana zitakuwa na maadili kama ya Arsenal, Liverpool na Man United ambapo kuna utaratibu wa miaka mingi kujenga wanasoka chipukizi?

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Klabu zakataa mfumo mpya Kombe la Dunia

Tanzania Sports

KLABU ZIKOJE TUNAPOELEKEA JUMA 20 LA LIGI YA ENGLAND ?