in

Ni duka la Yanga au GSM ?

Jezi mpya ya Yanga

Mzigo wa jezi za msimu mpya za klabu ya Yanga tayari ushafika. Jezi hizi zimeshaandaliwa mazingira mazuri ya kuuzwa. Moja ya kitu ambacho kimefanywa ni kuanzishwa kwa duka kwenye jengo la makao makuu ya klabu yaliyopo mtaa wa jangwani.

Mtaa ambao umebeba historia kubwa ya klabu ya Yanga. Ndiyo mtaa ambao uwanja wa Kaunda, uwanja unaomilikiwa na Yanga unapatikana.

Ndiyo mtaa ambao jengo la makao makuu ya Yanga ndipo linapopatikana kwa kiasi. Kwa sasa pamefanywa kuwa ndiyo mtaa ambao duka la jezi za Yanga ndipo linapopatikana.

Tanzania Sports
Jezi mpya ya Yanga

Kuweka duka kwenye makao makuu ya klabu ni kitu cha muhimu na msingi sana. Kuwepo kwa duka eneo lile kuna jenga imani ya kuwa jezi halisi za Yanga zinapatikana pale.

Utaratibu wa timu kuwa na jengo ambalo hutumika kama sehemu ya kuuza jezi  ni utaratibu ambao timu nyingi kubwa duniani huwa unatumia.

Kwenye viwanja vingi vya timu mbalimbali kubwa duniani huwa panakuwepo na duka ambalo huuza jezi za timu husika. Jezi zote hupatikana kwenye duka hilo.

Swali ambalo linazunguka sana tangu jana baada ya Yanga kuonesha kuwa wana duka katika jengo la makao makuu ya Yanga ni kuwa duka hilo ni la Yanga au GSM?

Kwanza Yanga wanastahili pongezi sana kwa kuwa na hili duka. Linapokuja suala la nani mmiliki wa duka kati yake na GSM nitaanza kukumbusha kitu.

GSM walishinda tenda ya  kubuni nembo ya jezi ya Yanga, kutengeneza na kusambaza jezi za Yanga. Lile duka lipo makao makuu ya klabu ya Yanga.

GSM itapata nafasi ya kuuza jezi zao kwenye duka lile.  Wafanyabiashara ambao hushinda tenda ya kubuni , kutengeneza na kusambaza jezi za timu kubwa hupewa na timu husika eneo la kuuzia jezi.

Adidas huuza jezi za Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford uwanja unaomilikiwa na Manchester United. 

Ndivo inavyokuwa na kwa GSM. GSM wao ndiyo watakuwa wanaratibu uuzaji wa jezi kwenye lile jengo na siyo Yanga. Yanga hawatahusika na uuzaji wa jezi kwa sababu pesa za jezi washapewa na GSM.

GSM walishatoa pesa za jezi kwa Yanga. Hivo GSM inabaki kuwa sehemu ambayo itapanga mipango mikakati ya uuzaji wa jezi ili kurudisha gharama zao ambazo wamewepa Yanga kwa mujibu wa mkataba wao.

Hivo hata siku ambayo mkataba wa GSM na Yanga utakapoisha na Yanga kuingia mkataba na Adidas basi GSM atatoa wafanyakazi wake kwenye hilo duka na Adidas ataweka wafanyakazi wake kwa ajili ya kuuza jezi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
£28m Ollie Watkins

Aston Villa walivyowazidi kete wapinzani EPL

Gareth Bale

Hawa ndiyo ‘maadui’ wa Gareth Bale Real Madrid