in

NGAO YA JAMII 

Septemba 25 Simba na Yanga zitapepetana kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es  salaam. Pambano la Ngao ya jamii ndilo utangulizi wa kufunguliwa pazia la Ligi Kuu Tanzania  Bara kwa msimu mpya wa 2021-2022.  

KWANINI YANGA NA SIMBA TENA? 

Pambano la Ngao ya Jamii linazipambanisha bingwa wa Ligi Kuu na mshindi wa kombe la FA  wa msimu uliopita 2020/2022. Lakini kwa vile bingwa alikuwa ni Simba ambao ndio vinara wa  Ligi Kuu Tanzania Bara, kanuni inasema timu iliyoshika nafasi ya pili kwenye kombe la FA ndio  itanyukana na bingwa wake kwenye mchezo wa Nago ya Jamii.  

HASIRA ZA YANGA 

Yanga wana hasira mara mbili kuelekea pambano hili. Kwanza wanakumbuka kipigo cha 1-0  kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA mkoani Kigoma. Mchezo huo unawapa hasira ya  kutaka kulipiza kisasi dhidi ya watani wao Simba. Ni chachu ya uzito wa mechi hiyo. 

Pili, Yanga wana hasira za kutolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa hatua za awali  baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 katika mechi mbili. Jijini Dar es salaam Yanga  walikubali kipigo cha 1-0 kisha jijini Port Harcourt wakapokea kipigo kingine cha 1-0 na  kuhitimisha safari yao ya mashindano ya kimataifa. Hivyo Yanga wanalazimika kusubiri hadi  msimu ujao kujua kama watashiriki Ligi ya Mabingwa au Kombe la Shirikisho. 

HASIRA ZA SIMBA 

Mabingwa hawa wa Ligi Kuu walizabwa katika mchezo wa tamasha lao. Ni tamasha la Simba  Day ambalo mashabiki walishuhudia mabingwa wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Afrika, TP  Mazembe wakioneshana ubavu na timu yao. 

Dakika tisisini zilimalizika kwa Simba kukubali kipigo cha 1-0 lililofungwa na Jean Beleke.  Kwa kukubali kipigo katika mechi ya tamasha lao kumeibua hasira ambayo ni lazima wajipoze  machungu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.  

Vile vile Simba wataingia uwanjani kutaka kuendeleza ubabe wao walioonesha mkoani Kigoma  kwenye fainali ya Kombe la FA, lakini wataingia uwanjani bila nyota wao waili Cletous Chama  aliyeuzwa Berkane na Luis Miquissone aliyouzwa Al Ahly ya Misri.  

KUTAMBIANA WACHEZAJI WAPYA

Katika mchezo huo timu hizo zinatarajiwa kutambiana nani amefanya usajili mzuri kuliko  mwingine. Simba watakuwa na nyota wao wapya kama vile Jeremia Kisubi, Deennis Kibu, Israel  Mwenda, Peter BandaSadio Kanoute, Pape Ousamane Sakho, Jimson Mwanuke, Abdulswamad  Kassim, Duncan Nyoni,Yusuf Mhilu, Henock Inonga. 

Yanga watakuwa na mastaa wapya, Djigui Diarra,Yannick Bangala,Herieter Makambo,Yusuf  Athuman,Jesus Muloko,Dennis Ambundo,Fiston Mayele,Djuma Shaban, Khalid Aucho,Eric  Johora. 

VITA VYA MAKOCHA 

Nasredine Nabi ana kibarua kigumu kuipa ushindi Yanga mbele ya Simba. Didier Gomes ana  kibarua kigumu kutetea ubabe wake mbele ya Yanga. Makocha wote wawili wanafahamu uzito  wa mchezo unaozikutanisha timu hizo. Kwa vyovyote mechi hii itakuwa na presha  kubwa,ubabe,ufundi na maarifa ya kutosha kutoka kwa makocha hao. ni mifumo gani itawafaa  kuibuka na ushindi kati ya iliyomo? Hilo litajibiwa katika mchezo husika.  

STAA MPYA 

Katika mechi kama hizi lazima kuna mchezaji anaibuka kuwa nyota wa mchezo. Staa huyo mpya  anakuwa amepachika bao au mabao au ni yule ambaye amefanya vitu adimu vitakavyobaki  akilini mwa washabiki. Kwa namna yoyote ile staa mpya ataonekana katika mechi hii. Lakini  haijulikani kama atakuwa ni kati ya wachezaji wageni waliosajiliwa na timu zote mbili au  atatokea katika kundi la wachezaji waliozoeleka. Ni vigumu kubashiri hapo. 

AJALI MCHEZONI 

Katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho ilitokea ajali ya mchezo kwa Mukoko  Tonombe kulimwa kadiri nyekundu baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Simba, John  Bocco. Ajali za namna hii za mchezaji kutolewa nje ya mchezo huchangia kwa kiasi kikubwa  kubadili mwelekeo,mbinu au upepo wa mshindi kwa timu. 

SIMBA KUWEKA REKODI MPYA? 

Simba ndio wamechukua ushindi wa mechi za Ngao za Jamii kwa miaka minne mfululizo tangu  mwaka 2017 hadi 2020. Rekodi zinaonesha kuwa Yanga wameshinda mara tano. Mwaka 2001  mshindi alikuwa Yanga. Mwaka 2002 na 2003 mshindi alikuwa Simba. Mwaka 2004 mechi hiyo  haikuchezwa. Mwaka 2005 mshindi alikuwa Simba. Mwaka 2006-2008 mechi hiyo  haikuchezwa. 

Mwaka 2009 mshindi alikuwa Mtibwa Sugar. Mwaka 2010 mshindi alikuwa Yanga. Mwaka  2011 na 2012 mshindi alikuwa Simba. Mwaka 2013 na 2014 mshindi alikuwa Yanga. Mwaka  2015 mshindi alikuwa Yanga. Mwaka 2016 msindi alikuwa Azam fc.

Takwimu zinaonesha kuwa Simba na Yanga zimewahi kuchukua kombe hilo mara tatu  mfululizo. Yanga walifanya hivyo mwaka 2013, 2014 na 2015. Nao Simba wakajibu mapigo  kwa kuchukua mara nne mfululizo mwaka 2017, 2018, 2019,2020. Na sasa wanafukuzia taji la  tano, na endapo watafanikiwa watakuwa wameweka rekodi ya aina yake tena mbele ya Yanga  ambayo haijashinda tangu mwaka 2015.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
SIMBA SPORTS CLUB

Viwanja 10 vibaya vya Ligi Kuu Tanzania 

Ligi Kuu Tanzania

MSIMU MPYA 2021/2022