in , ,

Newcastle waona mwezi

 

*Wawafumua Norwich 6-2

 

Newcastle wamepata ushindi wa kwanza katika mechi tisa za Ligi Kuu ya England (EPL), uliokuja kwa hasira, baada ya kuwapapatua Norwich 6-2 na kuwatia faraja washabiki walioanza kukata tama.

Ulikuwa ushindi wa aina yake Jumapili hii, ambapo Georginio Wijnaldum peke yake alifunga mabao manne na kutosha kuwanasua kwenye mkia wa msimamo wa ligi, lakini bado wanahitaji uendelevu wa hali hii mpya.

Licha ya kubadili kocha na kuajiriwa kwa Steve McClaren, Newcastle walianza vibaya msimu huu, ambapo katika mechi nane za mwanzo waliambulia pointi tatu tu, hadi Wijnaldum aliposhirikiana na Ayoze Perez na Aleksandar Mitrovic kufunga mabao hayo matano.

Norwich wenye pointi tisa na ambao ni msimu huu wamerejea EPL baada ya kushuka daraja misimu miwili nyuma, walijitahidi lakini wakazidiwa maarifa, ambapo mabao yao yalifungwa na Dieumerci Mbokani na Nathan Redmond, awali ikionekana kwamba wangeweza hata kutoshana nguvu.

Pengine hata McClaren hakuamini, mwenyewe kibarua chake kikionekana kuwa shakani kwa mwenendo hovyo jinsi hiyo, ambapo dakika 20 tu zilishuhudia mabao matano yakitikisa nyavu, matatu dhidi ya mawili ya washindwa. Ukweli ni kwamba safu za ulinzi hazikukaa sawa.

 

Advertisement
Advertisement

Kwa mfano, Mbokani alifanikiwa kufunga akiwa ndani ya yadi sita licha ya kwamba alikuwa akifuatiliwa vyema na Chancel Mbemba na Fabricio Coloccini, wakati Wijnaldum aliachwa kuruka mara mbili na kufungwa kwa kichwa huku Redmond akiwa hafanyi chochote kumzuia.

Norwich wangeweza bado kufunga mabao mengine mawili, kama si kwa mashuti ya Robbie Brady na Redmond waliokuwa wameachiwa na walinzi kugonga mwamba. McClaren ndio ushindi wake wa kwanza tangu awasili St James’ Park.

Newcastle wanashika nafasi ya 18 sasa, mbili juu ya Aston Villa wenye pointi nne na Sunderland wanaokokota mkia wakiwa nazo tatu na nakisi ya mabao 11 kwenye uwiano wa kufunga na kufungwa, huku Villa na Newcastle wakifungana kwa mabao -7.

Wijnaldum ni mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi, aliyesajiliwa msimu uliomalizika wa kiangazi kutoka PSV Eindhoven kwa pauni milioni 14.5 na kumfanya kuwa mchezaji wa tatu aghali zaidi klabuni hapo baada ya watangulizi wake, Michael Owen na Alan Shearer ambao wameshastaafu soka.

Katika mechi zijazo, kuna mazuri yanayoweza kuboreshwa, hasa ushirikiano mzuri uliooneshwa na mfungaji huo na Moussa Sissoko, na wanaweza kuwa tishio kwa timu nyingine, ikiwa kweli wamenyanyuka kutoka kwenye uvuli waliokuwa.

Wijnaldum anakuwa mchezaji wa pili kwa Newcastle baada ya Shearer kufunga mabao manne kwenye mechi moja ya EPL. Mitrovic naye aliyenunuliwa kwa pauni milioni 13 alionekana mwenye furaha kubwa, baada ya hatimaye kufunga bao la kwanza katika uwanja wa nyumbani.

Kocha wa Norwich, Alex Neil atakuwa katika matatizo, kwani hajaweza kupata ushindi kwenye mechi nne zilizopita za EPL na kuwa kwenye nafasi isiyo nzuri kwenye msimamo wa ligi. Ndio wanashikilia rekodi mbaya zaidi ya ulinzi kwa kufungwa mabao mengi na hakuna mechi hata moja waliyotoka bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa.

Wijnaldum anakuwa mchezaji wa saba wa Kidachi kufunga hat-trick kwenye EPL baada ya akina Dennis Bergkamp, Marc Overmars, Jimmy Floyd Hasselbaink, Ruud van Nistelrooy, Robin van Persie na Dirk Kuyt.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Manchester, Arsenal, Chelsea safi

Tanzania Sports

KUTAFUTA BALLON D’OR KWAANZA: